BINADAMU LAKINI MWILI SUMAKU!!

Ile hali ya kuwepo kwa binadamu walio tofauti na wengine inaendelea kuongezeka,kwani  huko  Croatia kaskazini mtoto wa miaka 6 aitwae Ivan Stoiljikovic ambaye amekuwa na hali ya kunasa vitu vya chuma (usumaku) katika kiwiliwili chake.Mtoto huyo ambaye pia kimwili umbile lake halilingani na umri,hilo halimpi halimzuii  kuvua chati na kuwaonyesha watu uwezo wake huo wa ajabu.
   Babu aitwae Ivan Surlovic anasema,alinza kuonesha maajabu tokea akiwa mdogo kwani  alianza kutembea akiwa na umri wa miezi nane,na kabla ya kufikisha miaka miwili alikuwa na uwezo wa kuendesha baiskeli,kitu ambacho kiliwashangaza.Babu yake anaendelea kusema, hali hiyo ya usumaku waligundua miezi michache iliyopita,wakati walipokuwa wakiangalia kipindi cha televisheni kilichokuwa kinamuonyesha kijana mwingine mwenye uwezo kama huo,nae Ivan ajijaribu kama utani, ghafla wakaona vitu vya chuma vinanasa pia kwake.
Familia yake inasema,hali hiyo huwa na nguvu zaidi nyakati za asubuhi akiwa ametulia,pia vyuma vizito hunanasa vizuri zaidi ya vile vyepesi.


Nzito lakini hapa ndo imenasa.

"Jamani ona mikono yangu ipo nyuma,sijaichika"

MUANGALIE HUYU JAMAA!!

Jamaaa mmoja ambaye hakufahamika jina lake,alifumwa akifuta viatu vyake kwa kutumia ulimi wake wakati akisubiri usafiri wa treni huko jijini New York.
Hizi ni picha za mshikaji akiwa katika harakati za kusafisha kiatu chake.

Check hii video yake uone vituko zaidi.

WEWE UNGEWEZA HII?


Check jamaa anavyomjali Ngamia wake!!hapa alikuwa anamfanyia medical checkup ya meno(pedicure).Daah sijui kama ingekuwa ni hapa nyumbani TZ kuna mtu angethubutu kufanya hivo?!
Kwa kawaida hapa Tanzania imezoeleka kwa wanyama hawathaminiwi ipasavyo.Kwa mfano pindi wanapoumwa maradhi au kupata tatizo la kuvunjika huwa wanaachwa bila msaada wowote.Kama ni mnyama anaelika basi huwa tunakimbilia kumchinja.

Huyu mwingine kaamua kumpeleka bata wake hospitali!!ingekuwa Kwetu bongo, KISU kingekuwa kinamuhusu bata na siyo hospitali!

Ulimwengu Jr & Princess washinda Mr & Miss UDSM 2011!!

Shindano la kuwatafuta Mr & Miss UDSM lilofanyika jana katika ukumbi wa Nkurumah,limemalizika kwa Jenerali Ulimwengu Jr kuchukua taji la Mr UDSM 2011 na kwa Miss UDSM mshindi ni Princess Chiaro.Washindi wengine ni Herieth Shija ambaye ni mshindi wa pili na na Anifa Issa ni watatu kwa upande wa mamiss.Mr UDSM na mbili ni Victor Hongoa na watatu ni Richius Kashonda.Katika mchuano huo mambo yalikuwa mazuri kwa upande wa Herieth Shija na Ulimwengu Junior kwani waliweza kunyakua tuzo za Miss & Mr Talents.Mshiriki mwingine aliyedhaniwa kuibuka kidedea ni Raheem Mkadara a.k.a Da Prince lakini upepo ulikuwa vibaya kwa upande wake na kuambulia kuingia Top five tu.!
Washindi wa Miss UDSM 2011 katika pozi la pamoja.Kushoto ni Herieth Shija mshindi wa 2,kulia ni Anifa Issa (3) na katikati ni Miss UDSM

Mr UDSM, Jenerali Ulimwengu Jr katika vazi la ubunifu.


Miss UDSM  2011 akivikwa taji.


Mr UDSM wakati wa kujibu maswali.
Kwa habari na matukio yaliojiri siku hiyo  bofya Photo Album page hapo juu.Picha na Hilal Ruhundwa 

TIBA JINGINE JAMANI!!

     Azerbaijan  ni moja ya nchi zinaongoza kwa uzalishaji na uuzaji mafuta dunia. Katika mji wake mkuu Baku, kumetokea hospitali inayojulikana kwa jina la Naftalan ambayo kwa miaka mingi sasa imekuwa ikitumia mafuta ghafi kama tiba ya magonjwa  mbalimbali ya ngozi  na mengine ya viungo na mifupa kama arthititis na rheumatism .  Katika tiba hiyo mgonjwa hutakiwa kujiloweka katika sinki lenye gallon 35 za mafuta hayo na kukaa ndani yake kwa muda usiozidi dakika kumi.Wagonjwa wengi wamesema hujisikia vizur wakati wapo ndani ya mafuta hayo hivyo kutamani  kukaa zaidi ya dakika hizo zinazopendekezwa na daktari. Meneja mkuu katika hospitali hiyo, Dr Alif Zulfugar amesema kuwa mgonjwa hatakiwi kuzidisha dakika pia haruhusiwi kutumia tiba hiyo zaidi ya mara moja kwa siku kwani inaweza kumletea madhara ambayo hakuyataja.Ameongeza kwa kusema tiba hiyo inatolewa kwa muda wa siku 10 tu.

Baadhi ya wagonjwa wakioga dawa hiyo




Jamaa akifutwa mafuta hayo baada ya kujiloweka


OSAMA AUWAWA.

 Rais Barrack Obama amethibitisha taarifa za kifo cha Osama Bin Laden,kiongozi wa kundi la Al-Qaeda ambaye ameuliwa katika operesheneni iliyofanywa na majeshi ya Marekani jana jumapili huko Pakistan katika mji wa Abbottabad.Kufutia taarifa hizo Obama amehaidi kuimarisha ulinzi katika Balozi zao kwani ana wasiwasi wa kutokea mashambulizi.
Osama enzi za uhai wake akiwa na viongozi wengine wa Al- Qaeda

Wamarekani wakishangilia taarifa za kifo cha Osama.

WANAWAKE HAWA JAMANI!!




Inashangaza kuona wanawake hawa kunyonyesha wanyama.!!

MPAKA KIELEWEKE!!

"Kitafahamika tu!!" Hayo ni maneno ya Binti wa Kijerumani Regina Mayer, ambaye kwa muda mrefu alikuwa na ndoto ya kuendesha farasi lakini haukweza kufanikiwa kwa wazazi wake hawakumwezesha kutimiza ndoto zake. Basi ndipo binti huyo wa miaka 15 alipoamua kumfundisha ng'ombe wake aitwae LUNA kuruka viunzi kama farasi.

MATOKEO KIDATO CHA SITA YAMETOKA.

Matokeo ya kidato cha 6 2011 yametoka,kwa habari zaidi bofya www.necta.go.tz/2011/alevel.htm

MACHAFUKO BAADA YA UCHAGUZI HUKO NIGERIA

Kumetokea machafuko ya kisiasa huko kaskazini mwa Nigeria baada ya kutangwaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi, matokeo hayo yameonyesha Bw Goodluck Jonathan amemshinda mpinzani wake Bw Muhammadu Buhari. Vurugu hizo zimepeleka vifo vya watu sita na wengine kukimbia makazi yao. Taarifa zaidi zinaonyesha uwepo wa vifo vingi na hali kuwa mbaya zaidi.Machafuko yameshika kasi sana katika miji ya Kaduna na Kano.
Wananchi wakifanya vurugu huko Nigeria kaskazini

                                                                                       from aljazeera

NJIA ZA WAENDESHA BAISKELI

Huko London wenzetu wamepiga hatua kwa kuandaa njia maalum kwa waendesha baiskeli,njia hizo zimepakwa rangi ya blue.Njia hizo zimeanza kuwekwa huko West London,mikakati yao kufikia 2015 mji wote utakuwa na njia hizo.

KIBOKO WA RANGI YA PINKI

                             Umeiona hii??kiboko huyu anapatatikana Kenya.

HATIMAYE GBAGBO AKAMATWA.

Baada ya kung'ang'ania madaraka kwa muda mrefu,rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amekamatwa na jeshi la nchi hiyo kwa ushirikiano wa jeshi la umoja wa mataifa Ufaransa.Wakilishi wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa amesema  Gbagbo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Rais Gbagbo akitolewa nje ya hoteli alipokuwa amejificha

Mwanajeshi akishangilia ushindi wa kumkamata Gbagbo
                           Mke wa Gbagbo,Bi Simone nae awekwa chini ya ulinzi

THE GAME NDANI YA KIJOGOO

Msanii The Game nae ameamua kutupia style ya Kijogoo a.k.a  KIDUKU kwenye kichwa chake.Style hii hapa nchini inapendwa sana na wasanii kutoka THT

VIKOMBE VYAZIDI KUTOLEWA!!!

Baada ya Mchungaji mstaafu Bw Ambilikile Masapile"BABU" kuja na dawa inayotibu magonjwa sugu "KIKOMBE" kaoteshwa na MUNGU.Sasa kumeibuka watu wengine wanaogawa dawa kwa mtindo huo wa KIKOMBE nao wanadai wameoteshwa!!

Babu akifanya vitu vyake.
Mfano huko Tabora amejitokea mwanamke anaetambulika kwa jina la Magret Mutalemwa a.k.a BIBI nae anagawa kikombe kwa madai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria,tofauti na BABU,BIBI anatumia kikombe cha udongo huku akikushika kichwa wakati anakupa kikombe.Wagonjwa mbalimbali wametoa shuhuda za kupata nafuu baada ya kupata kikombe cha Bibi,huku wakiitaka serikali kupitia halmashauri ya Tabora kumsaidia BIBI kutoa huduma hiyo kwani mazingira ya kufika kwake sio mazuri.
                              bibi na kikombe chake.

Halikadhalika huko Pwani maeneo ya Ruvu Darajani amejitokeza kijana Juni Abunda aliyepewa jina la KAKA,nae anagawa kikombe kinachotibu magonjwa sugu kwa madai ya kuoteshwa na Mungu.Kaka yeye anatoa kikombe bure!!!
Wakati huohuo ahuko Mbeya Mchungaji Mwasumale wa kanisa la kinabii lililopo Tukuyu Rungwe nae anatoa kikombe.Mbali na hao Morogoro nako amejitokeza mwanamke mwingine anayeitwa Fatma Senga nae anagawa kikombe.Sasa sijui huyu ataitwa nani?? labda Shangazi.

PICHA YA WATOA KIMAISHA!!

Kwa miaka 11, Rozonno na mkewe Mia McGhee walifanya kila walichokiweza ili waweze kuzaa mtoto angalau mmoja,hatimaye mwaka jana mwezi juni Mia alifanikiwa kupata mimba na kujifungua si mtoto mmoja bali watoto mapacha sita

Lakini mahitaji ya watoto hao wachanga yalikuwa makubwa kuliko uwezo wao. Kwa siku watoto hao walitumia jumla ya nepi 50 na chupa 30 za maziwa
Mia alimwambia mumewe waweke pozi na watoto wao na walipiga picha ambayo Mia aliiweka kwenye mtandao wa Facebook kwani maombi yao ya msaada kwa manispaa yalikataliwa.

Picha hiyo ilijipatia umaarufu duniani na haikuchukua muda ilimfikia bilionea Oprah Winfrey ambaye alivutiwa na picha hiyo na kuamua kumualika Rozonno na mkewe kwenye shoo yake pia Oprah aliizawadia familia hiyo dola 250,000 za kufanya manunuzi ya mahitaji yao yote wakati wowote wanapotaka kwenye mtandao wa supermarket kubwa Marekani ya Walmart.

Ingawa Rozonno na mkewe walishaoana miaka 11 iliyopita walipokuwa na umri wa miaka 18 na 19, Oprah aliwazadia zawadi ya kwenda fungate (honeymoon) kwenye mojawapo ya hoteli kubwa za mjini Las Vegas.

KUDUME CHA DUNIA.

Huyo si mwingine bali ni mzee Ziona Chana mwenye  miaka 67 ambaye pamoja na kuwa na wake 39, watoto 94, wajukuu 33 lakini bado ana mpango wa kuongeza wake wengine zaidi ili kuikuza familia yake.Familia nzima ina watu 181 inaishi kwenye nyumba moja kubwa ya ghorofa nne yenye  vyumba 100 iliyopo katika kijiji cha Baktwang katika jimbo la Mizoram nchini India.

Msosi wa usiku mmoja pekee unapoandaliwa ni sawa na maandalizi ya sherehe fulani kwani jumla ya kuku 39, kilo 60 za viazi na kilo 100 za mchele hutumika ili kuitosheleza familia nzima kwa usiku mmoja tu achilia mbali chakula cha mchana na brekfasti


Mwenyewe ajigamba kuwa mwanaume mwenye bahati kwa kumiliki   wake 39 na kuwa mkuu wa familia kubwa kuliko zote duniani.

       Mjengo wa mzee Ziona ambapo anaishi na familia yake

Hiki ni chumba za wake zake kwani yeye huishi kwenye chumba cha peke yake  ambapo wake zake 39 hupeana zamu za kulala ndani ya chumba hicho na mzee huyo wa kaya.


WAZEE WA KAZI..

Nani anaebisha kwamba hawa jamaa,wameitingisha nchi yetu kisiasa??Mkumbuke Mzee Lyatonga enzi zake miaka ya 90 na Dr Slaa kipindi hiki na kizazi cha dotcom.

LIBYA PIA HAPATOSHI!!!

Lile vuguvugu la kisiasa limeendelea kuzikumba nchi za Afika ya Kaskazini,kwani leo katika mji wa Benghazi nchini Libya, kumetokea maandamano ya maelfu ya watu wanaopinga utawala wa Rais Gaddafi.