Zaidi ya watu sitini wamefariki
na wengine mia mbili kujeruhiwa katika pwani ya Ivory coast katika sherehe za
kuukaribisha mwaka mpya.
Baadhi ya nguo zilizobaki baada ya mkasa huo |
Kisa hicho kilitokea kufuatia
msongamano wa watu wakati wa sherehe hizo, za kuukaribishwa mwaka mpya wa 2013.
Vyombo vya habari vya taifa
hilo vinasema tukio hilo lilitokea mapema alfajiri katika jiji kuu la Abijdan.
Inasemekana kuwa watu hao
walikuwa wakishuhudia maonyesho ya fataki katika uwanja wa michezo.
Wengi waliofariki ni watoto
kati ya miaka minane hadi kumi na mitano.
Hata hivyo haijulikani
kilichosababisha msongamano huo.
Ajali hiyo ilitokea katia
uwanja wa michezo wa Felix Houphouet Boign, ambao una ukumbwa wa kuruhusu
mashabiuki elfu sitini na tano wa soka na ulipewa jina hilo kama heshima ya
rais wa kwanza wa nchi hiyo.
Kabla ya ajali hiyo uwanja huo
uliandaa maonyesho ya muziki iliyohudhuriwa na mwana muziki kutoka Marekani
Chris Brown.
from BBC Swahili