MKASA MZIMA WA IFM #poleni sana

Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga.

Picha hii inakuonesha kwa karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata fikiria kama huyu askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi, Je! Wale waliopata mkong'oto wapo kwenye hali gani?


Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo


Kundi la wanafunzi walishikwa kama kuku wa mdondo baada ya kupigwa mabomu ya machozi na kujikuta wakijificha sehemu moja kundi zima hali iliyosabisha kutembezwa kichurachura hadi kwenye kituo cha Polisi cha Kigamboni.


Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi



Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigo vile alivyojiskia ili amalizie hasira zake.

Askari huyo aliendelea kutoa dozi

                                   ANGALIA PICHA HIZI TATU KWA MAKINI


Alianza kwa kupandishwa kwenye gari

Ghafla alidondoka kwenye gari la polisi baada ya gari hilo kujaza wanafunzi wengi

Gar liliondoka yeye akaachwa chini

    Sijui kama dada huyo alisalimika kweli?
picha kwa hisani wavuti.com