Naamini bara la Afrika ni moja ya sehemu iliyobarikiwa sio tu kwa rasilimali zilizopo bali pia kuwa na watu wenye nguvu kuliko sehemu nyingine duniani. Lakini cha ajabu ndio sehemu inayoongoza kwa matatizo kama vita (vurugu),ufukara,ufisadi,njaa na ukame kuliko sehemu yoyote.Sijui tatizo letu ni nini??. Wapo wanaosema eti WAAFRIKA TUMELAANIWA!! Mimi siamini kwamba tumelaaniwa kwani Mungu hawezi kuwa katili na muonevu kwa Waafrika kiasi hicho,tatizo lipo sehemu limejificha,kuzungumzia LAANA ni uvivu wa kufikiri na uwoga wa kuumiza kichwa katika ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili.
Kwa upande mwingine inaniingia akilini kwamba yaweza kuwa laana,tena iliyotoka kwa shetani, hii inatokana na matendo yatunayofanya waafrika. Mfano mzuri ni hali inayoendelea huko pembezoni mwa afrika katika nchi ya Somalia,kwa muda wa miezi mine sasa imekumbwa na ukame na njaa illiyosabisha njaa kali kwa wananchi na mifugo yao. Hali hii imesababisha vifo vya mamia ya watu hasa watoto na wengine maelfu kukimbilia nchi za Kenya na Ethiopia kama wakimbizi.