Homa matokeo kidato cha 6...sintofahamu yazidi kwa watoto wa wakulima


Zikiwa zimebakia siku chache kwa matokeo ya kidato cha sita 2012 kutoka, homa”   juu ya hatima ya vijana waliofanya mtihani huo imezidi kuongezeka. Joto hili limezidi kuongezea sio tu kwa kuhofia ufaulu wa mtihani yao bali kilichoongeza sintofahamu ya  hatma yao kwenda vyuoni, wengi wahofia kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu kwani hali ya kupata ufadhili kutoka bodi ya mikopo (HESLB) umeanza kuonekana  kuwa mgumu (tete).

Kukata tamaa huku kumechangiwa zaidi na taarifa zilizotolewa na TCU kupitia kitabu cha mwongozo wa udahili 2012/2013-Admission guide book 2012/2013. Katika kitabu hicho ambacho licha ya kutoa vigezo vinavyohitajika ili mwanafunzi achaguliwe kwenda kusoma katika chuo husika pia wametoa mchanganuo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013. Katika mchanganuo huo  unaonyesha vipengele viwili ambavyo ni Possible Loan amount na Loan Priority. Katika kipengele cha loan priority kinaonyesha kozi (taaluma) ambazo zimepewa kipaumbele cha kupewa mkopo, hivyo kupelekea kuwepo kwa makundi mawili ambayo ni Priority na Non Priority. Kwa ufupi non priority ni wale ambao hawana uwezekano wa kupata mkopo. Hivyo possible loan amount kinawahusu wale ambao ni priority (watakopata mkopo)

Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba asilimia 96 ya kozi zote zinazotolewa na vyuo mbalimbali ni non priority isipokuwa kwa wataochagua Education, Engineering na Medicine,Kilimo na kozi nyingine baadhi za sayansi. Hiki ni kizungumkuti kwa wale waliokuwa na matumaini ya kusoma Biashara, Uchumi, Political Science, Sheria, Uandishi wa Habari, na kozi nyingine zilizobaki kwani upatikanaji wa mikopo kwao ni ndoto. Sijui ndugu zangu watoto wa wakulima waliosoma EGM, HGE, HKL, HGL, HGK KLF nk watakimbilia wapi? Kimbilio liliobaki ni education pekee, tena watakaomudu kusoma hii  ni wale waliotoka kwenye familia zenye auheni kidogo (middle class) kwani bodi wanatoa ufadhili wa 50% kwa watakaosoma education;  lakini kwa mtoto wa mkulima choka mbaya kupata elimu ya chuo asahau.

Wazee wa IFM  mpo??chuoni kwenu hakuna kozi hata moja inayokula mkopo??
Uwezo wa kumudu gharama za ada, (tuition fee), chakula na malazi (meals & accommodation), na fedha nyingine za kujikimu zitapatikana wapi? Gharama hizi mzigo usiobebeka na wazazi wengi hawawezi kumudu gharama hizi. Hiki ni kilio, tena kisicho na mfiwa maalumu..wafiwa ni watoto wa masikini ambao ni tuko wengi hapa Tanzania. Kwa hali hii watakaosoma vyuo ni watoto wa matajiri tu! watoto wa wakulima twende wapi?  kwenye mabenki tukachukue mikopo ya kujisomesha? Inasikitisha kuangalia kitabu hicho cha TCU. 
Hii ni chinja chinja mpaka wazee wa Mzumbe panga hili limewapitia
Nashindwa kuelewa nini maana ya mkopo?hivi fedha hizi si hurudishwa pindi mwombaji anapomaliza masomo? Au ndo serikali haina fedha kama tunavyosikia? Huku ni kutowatendea haki watoto wa masikini walio na kiu ya kupata elimu ya juu. Tena ni uonevo mkubwa..njooni vyuoni mtazame maisha ya wanafunzi wa mwaka jana waliokosa mkopo..maarufu kama NO LOAN…nadhani kupitia hili umuhimu wa kuwapatia wanafunzi mikopo unaweza kuonekana. 
Sio kwenu tu IFM ndo hakuna mkopo?vyuo kibao kama CBE,Ustawi, Tumaini,KIU,bodi hawatoi mkopo pia



Matokeo hayo ya kidato cha sita yanatarajiwa kutoka mwisho mwa mwezi huu kama ilivyo ada. 
Wazee wa SUA

HILL mpo??