Ugonjwa wa Dk. Mwakyembe Januari 3, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiffCdsF7FyQ7JRUTa0yJJ4pz6GIKVljMgiFS7n_D4czGWqLLMJoRko78YW6-98n_ck4MZZZHo9U43uIbYtcq81hs4xa77bHhEUW3RaOrPe7cW9DvjGLDNJaMHlKhR3pkSwKsOh2iqlw5uh/s200/mwakembe.jpg)
Madaktari 229 wafukuzwa
Muhimbili Januari 6, 2012
UONGOZI
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) uliwafukuza kazi madaktari 229 waliokuwa
katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo wa siku nne wakishinikiza
kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Umeme bei juu Januari
14, 2012
WAKATI
gharama za maisha kwa Watanzania wengi zikizidi kupanda kila siku, Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), iliidhinisha ongezeko la bei ya
umeme kwa asilimia 40.29 kwa Tanzania Bara na asilimia 28.21 kwa Zanzibar
kuanzia Januari 15, 2012.
Madaktari waanza mgomo nchi
nzima Januari 23, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijMHmXAgZtRo-LLDf3zsA9YWxmrSJWEuxAkn67hpY3_Q7f1eedNrMKoal7MNjHtTFNoqJUF4LvzEldFirjhp-a6qlUdB3J5GT_L5I4g19PY_L6Q7bXUQ5cNpATmmFd9FLBhqgqj2yD4-0i/s320/wauguzi.jpg)
Mwenyekiti
wa Kamati ya Madaktari, Dk. Ulimboka Stephen, alisema mgomo huo ungelikuwa wa
nchi nzima kwa madaktari kutotoa huduma.
Wanafunzi wanane wafa maji
Arusha Februari 28, 2012
WANAFUNZI
wanane kati ya kumi wa Shule ya Msingi Piyaya, wilayani Ngorongoro, mkoani
Arusha, walifariki baada ya kusombwa na maji ya mafuriko ya Mto Radiru wakati
wakitoka shuleni, jioni majira ya saa 11:30.
Mei 3, 2012 Watu
saba wafa ajali ya basi la NBS
WATU
saba walikufa papo hapo na wengine 54 walijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya
NBS lenye namba za usajili T 978 ATM lililokuwa likitokea Tabora kuelekea
Arusha kupinduka katika eneo la Jineri, nje kidogo ya mji wa Igunga.
Dk. Ulimboka atekwa na
kupigwa Juni 28, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYDS5XsVgT1B6FcLcwbu22I2xnB27eGIySEACfilzntjEBJocPoZHylG4KS6lrDFHV3ipVBH7E35cMpWezijtE_Zr20zVFjdNGxx8vOjm426lYBZhcw3t8wRsq__mgi44fBOy2SE3y8x55/s320/Ulimboka2.jpg)
Serikali yawashtaki
madaktari Julai 7, 2012
SERIKALI
iliwashtaki katika Baraza la Madaktari Tanzania, madaktari wanafunzi wa vitendo
walioshiriki kwenye mgomo wa madaktari uliofanyika nchini kwa tuhuma za
kuhatarisha maisha ya wagonjwa na kukiuka maadili ya taaluma yao.
Meli ya Mv Skagit yazama Julai
18, 2012
Sheria ya mifuko ya jamii
moto Julai 27, 2012
VUGUVUGU
la kupinga mabadiliko ya sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2012
lilichukua sura mpya baada ya wabunge kutaka kuifanyia marekebisho mengine kwa
sababu mwanachama hataruhusiwa kuchukua mafao yake kwa sababu yoyote mpaka hapo
atakapofikisha miaka 55 au 60.
Ugonjwa wa ebola waingia
nchini Agosti 5, 2012
UGONJWA
hatari wa ebola ambao umeua idadi kubwa ya watu nchini Uganda uliripotiwa
kuingia nchini katika wilaya ya Kyerwa, kijiji cha Bulongo, mkoani Kagera,
ambapo mtoto wa miaka sita alionekana na dalili hizo.
Walimu watishia kuing’oa
CCM Agosti 6, 2012
WALIMU
walipokubali kurejea kazini na kuendelea kutafakari amri ya mahakama, mkakati
mzito ulipangwa kuhakikisha hawakiungi mkono Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye
Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Mauaji ya Daudi MWANGOSI Septemba
3, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9CWaFBY1jAGyrhCYh6o9MqIdgVzc0fxf6I7lHhn4reimL9QO4s2gRclTG0rj_ClV5zliancHkC83esYGNt8abY0fzdlg4npZmaOHJQjYMZ2V13Z_LEz9WzWvJRFvEaiIZM9QJ_NP0nLMV/s320/mwangosi.jpg)
Mwangosi
alidaiwa kuuawa kwa bomu lililorushwa na polisi waliotaka kuizuia CHADEMA
kufungua tawi katika kijiji cha Nyololo.
Waislamu waandamana Dar Septemba
21, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgP01p4WQjI-Ix0YgHkOHLeYaJ_czaexpNFtZTujdInTd-JCNKVxn1IF9MijAqbCd54VtLMJWcBffhai5KSabSEWnbySYCNyWibCiv0krtAmE33Yb9YCLMntRff6_3vVgR63l7d3BAxXvGy/s320/01.jpg)
Ajali yaua 10 Mbeya, mbunge
anusurika Oktoba 3, 2012
MBUNGE
wa Viti Maalum Mbeya kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mary
Mwanjelwa, alinusurika kufa katika ajali iliyogharimu maisha ya watu takriban
10.
Ajali
hiyo ilitokea eneo la Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini. Gari la mbunge huyo
liligongwa na kuteketea kwa moto papo hapo.
Kizaazaa
cha mafuta Dar Oktoba 3 2012
MAMLAKA
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) baada ya kushusha bei za
mafuta ya petroli na dizeli nchini, baadhi ya wafanyabiashara walizua kizaazaa
kwa kuweka mgomo baridi wa kuuza mafuta hayo.
Waislamu wachoma, wavunja makanisa Oktoba 12, 2012
KUNDI
kubwa la Waislamu wenye imani kali, lilizusha vurugu kubwa zilizoambatana na
kuchomwa moto na kuharibiwa makanisa manne huko Mbagala jijini Dar es Salaam,
katika kile kilichoelezwa kuchukizwa na kitendo cha kijana mmoja wa Kikristo
aliyedaiwa kukimwagia haja ndogo kitabu kitakatifu cha Kurani.
Ponda akamatwa kwa
uchochezi Oktoba 17, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_F1YY1JyYm8w5-PMq_wUWd8D51twHR1tuJ3SPJlkAtSwtCOX5keV9Df7Ak1F8Tg937NF0mGqKWGxMmHAqehLKvAT6zM2yepnJBfftQFLSK0RwR9gOHyX8KbEkFiajW20v-DL_h_YK6ZRc/s320/144.jpg)
Padri apigwa risasi
Zanzibar Desemba 26, 2012
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjB9EZ_kFT2stV4Fa4RnDCdjoSyV3tck00uiWkLxnq4IRwmXuy_rJAJpiN_R3yqFmJFaodCCHZBNgBeIG_tEd1Ss_TKRQ3B4XI1x2fHZMyxDDUoPs0cWz3U8s1qVfOkwV-5YiSLrOTtVuP/s320/pedre.jpg)