Wanaume nchini Kenya waandaa mgomo wa kutokula majumbani mwao!!

Kufuatia malamimiko ya muda mrefu ya kupokea kipigo kutoka kwa wake zao, wanaume nchini Kenya wamepanga kufanya mgomo wa kutokula majumbani mwao kwa muda wa wiki moja. 
kiAtoa rai hiyo Kiongozi wa chama cha kutetea wanaume Bw Nderitu Njoka amesema,badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni.
Aidha Bw  Nderitu amesisitiza kuwa kuanzia leo jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akina baba kula mahotelini badala ya majumbani mwao.Ameongeza kuwa mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.
Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wauaume alikuwa akizungumza katika hospitali kuu ya mjini Nakuru huko Rift valley ambako alikuwa amekwenda kumjulia hali baba mmoja ambaye amelezwa  kutokana na kipigo alichopewa na mkewe.
Bw Njoka akimpa pole baba aliepigwa na mkewe
Baba huyo akizungumza kwa uchungu hospitalini alisema mkewe alimuita nyumbani ili akachukuwe pesa kabla ya kumfungia chumbani na kumtandika.
Kwa mujibu wa bwana Nderitu Njoka, mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopigwa na bibi zao. Katika mkoa huo wa kati wanaume karibu nusu milioni wameripoti kupigwa na wake zao. Chama hicho cha wanaume kimedai kuwa kuna wanaume ambao wanalazimishwa kufua nguo za wake zao. Wengine pia wamelalamika kunyimwa tendo la ndoa na mabibi zao.
Jijini Nairobi wanaume ambao huona kivumbi kutoka kwa wake zao ni laki tatu.
Lakini baadhi ya akina mama kutoka mkoa huo wanasema akina baba ndio wa kulaumiwa kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ya kifamilia.
Wanasema waume wengi wamekuwa "wanaume suruali" tu.
Hata hivyo wengi wanasubiri kuona kama kweli mgomo huo utafaulu, na ni wanaume wangapi walio na pesa za kwenda kula hotelini badala ya kula majumbani mwao.

source bbc swahili