SIRI YA MGAO WA UMEME NCHINI HII HAPA


   Kwa  muda mrefu sasa hapa Tanzania tunakabiliwa  na tatizo la mgao wa umeme bila kujua chanzo chake ni nini wala mwisho wake ni lini. Kama mmoja wa waathirika wa tatizo hili,wakati nikitafakari kuhusu tatizo hili, kwa kuona uzito wake, nikasema sio  bure  labda nchi yetu na shirika la umeme TANESCO  wamelogwa!!nikaona HAPANA kwa waganga tulionao hapa nchini ufumbuzi  ungekuwa umeshapatikana mapema. Ghafla nikapata jibu kwamba shirika la TANESCO limelaaniwa! ndiyo limelaaniwa. Sasa laana hii imetoka wapi? Nikakumbuka  ule mgogoro wa TANESCO na Askofu Zachary  Kakobe kuhusu kupitisha kanisani kwake nguzo za umeme zenye kilovoti 132 uliojitokeza mwanzo mwa mwaka 2010, Askofu Kakobe pamoja na wamumini wake walikesha na kufunga  kwa maombi ili nguzo za Tanesco zisipite kanisani kwako  lakini Tanesco walitumia nguvu ya serikali wakapitisha nguzo, Kakobe hakuridhia uamuzi ule na aliahidi kuuendelea na maombi  ili  kuwaaibisha TANESCO na aliongeza kuwa kwamwe hawataweza (TANESCO) kushindana na Mungu, (baba wa sayansi zote). Mungu hawezi kupuuzia sala na maombi ya wale Vikongwe waumini na Kakobe waliokesha usiku na mchana kulinda kanisa lao ili TANESCO wasipitishe nguzo. HAKIKA SASA MAOMBI NA SALA ZA MTUMISHI WA MUNGU KAKOBE zimesikika MBINGUNI, TANESCO imeshindwa kabisa kutatua tatizo la umeme nchini.

Askofu Kakobe wakati wa mgogoro wake na TANESCO mwaka jana
      Kudhihirisha hilo kuwa laana hii yatoka kwa MUNGU kama alivyosemwa katika maandiko “nitakulaani wewe na vizazi vyako vyote” ni kweli sasa imekuwa sio kwa TANESCO tu, bali laana hii imeenea kwa wizara yote ya nishati na madini. Angalia mgogoro wa ukosefu wa mafuta nchini uliojitokeza hivi karibuni, kutoelewana kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na EWURA, kusimamishwa kazi kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini  Bw Davis Jairo na hata kupingwa kwa bajeti ya wizara kutokana na tatizo la umeme. Yote haya yanadhihirisha kwa kizazi chote cha wizara ya nishati na madini vimekumbwa na laana hii. 

Tatizo la mafuta lilivyojitokeza hivi karibuni.
     Ili kuondokana na haya yote, TANESCO wamrudie Kakobe na  awaongoze kwa sala ya toba. Kama walivyofanya kipindi kile cha mgogoro, Waziri Ngeleja na serikali kwa ujumla itawalazimu tena wamrudie mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe ilikupata baraka zake, la sivyo tatizo la umeme litaendelea licha ya serikali kuonyesha nia ya dhati ya kutatua tatizo hili.
Askofu Kakobe na Waziri Ngeleja wakati wa  mgogoro kuhusu  wa uwekaji nguzo.

TCU YATOA TAMKO KWA FORM SIX LEAVERS.


  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewataka wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kupitia tume hiyo kuwa na uvumilivu kwani majibu yatatoka hivi karibuni.

   Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Uhusiano wa TCU, Edward Mkaku, alipozunguumza na gazeti la NPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi walioomba nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwamba tume imechelewa kutangaza majina.

   Mkaku alisema kwa kawaida matokeo ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini hutolewa mwishoni mwa Julai. Hata hivyo, alisema mwaka huu majina yamechelewa kutangazwa kwa kuwa Seneti za vyuo zimechelewa kufanya vikao kwa ajili ya kupitia na kuhakiki majina na sifa za walioomba.

   Alisema kazi ya TCU ni kuratibu na inapomaliza humuita Afisa Msajili wa kila chuo kwenda kuangalia kama wanafunzi waliochanguliwa wana vigezo vya kujiunga na chuo husika kwa kuwa kila chuo kina kuwa na vigezo vyake. Baada ya kila Afisa Msajili kuhakiki vigezo vya waliochanguliwa, huenda kukaa na Baraza la Seneti la kila chuo kuhakiki tena vigezo hivyo na baada ya hapo majibu yanarudishwa TCU.

  Akasema TCU ilikutana jana na wakati wowote itatoa majibu ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu.

Alisema TCU ina mawasiliano ya vyuo hivyo ambavyo ni taasisi huru.

from,wavuti.com