Field hazishikiki!!Ajira hazionekani!!huu msiba unakuhusu..

   Kweli daima itatuweka huru, inashangaza kuona  malumbano juu ya kauli ya iliyotolewa hivi karibuni na waziri mkuu mstaafu Mh, Edward Lowassa kuwa tatizo la ajira nchini ni bomu linalosubiri kulibuka!!Kiukweli nashindwa kuelewa yanatokea wapi kwani tatizo hili liko wazi kabisa..nashawashangaa pia watu wanaojitahidi kupindisha ukweli katika hili ilhali ukweli unajulikana..cha kusikitisha kada wa Umoja wa Vijana CCM anathubutu kumkejeli Mh Lowassa eti aonyeshe mikakati alioifanya kupunguza tatizo la ajira wakati alipokua waziri mkuu!!Hii ni kejeli na mzahaa usiotakiwa wakati mambo yanayougusa umma yakijadiliwa. Au ni kwa sababu tu Lowassa ndo amezungumza basi imekua nongwa?!!Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..Kiukweli ajira ni issue (tatizo), tena sio bomu linalosubiri kulipuka bali tayari limeshalipuka na  kilichobaki ni kuona madhara yake.

  Katika kudhihirisha kuwa tatizo la ajira nchini ni kubwa kwanza tuanze kuangalia namna ya upatikanaji wa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) kama inavojulikana kwa wengi. Kwa utafiti mdogo uliofanywa katika vyuo vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria, College Business Education imebanika kuwa kati ya wanafunzi kumi,saba kati yao wamekiri kabisa kukosa nafasi za field sio tu kwenye taasisi binafsi hata zile za serikali. Ugumu huu umekua kikwazo sana kwa wanafunzi wanaosoma taaluma nyingine tofauti na ualimu kwani upatikanaji wao huwa ni rahisi kwani vyuo vingi mawasiliano na shule husika ambazo wanafunzi wanataenda kwa ajili ya mafunzo.

   Sababu husika ya ukosekanaji wa nafasi hizi imebainika kuwa ni urasimu uliopo kwenye taasisi hizo. Mwanafunzi unaweza kupeleka barua kwenye ofisi na barua hiyo isipokelewe kabisa na unapewa majibu kwamba hapa hatunaga mambo hayo..yaani hawapokei wanafunzi wa field..kwingine barua inapokelewa lakini majibu hayatolewi unatafutilia kutwa kucha mwishowe watakujibu we don’t have the chance to accommodate you!! Kwingine utambiwa samahani barua yako haionekani jaribu kuileta tena..Kiukweli hali hii inakatisha tama kwani mwanafunzi huzunguka hadi muda wa miezi miwili bila mafanikio. Pia kuna baadhi ya ofisi ambazo zinajulikana kabisa kuwa chuo fulani hakipokelewi kwa nafasi za field..utajibiwa hapa hatupokei Open na Ustawi nafasi zipo kwa vyuo vingine…Tukapate wapi hayo mafunzo kwa vitendo wakati nafasi zenye hazipatikani? Chakujiuliza kama field ni zengwe kiasi hiki je hizo ajira inakuaje??ni wazi kwamba hata ajira ndo hazionekani kabisa.

   Kudhihirisha kuwa hili tatizo ni kuna baadhi ya watu wamegeuza deal na kufungua ofisi ambazo huwaunganisha wanafunzi na ofisi ambazo watahitaji kwenda kufanya field. Ilikumwezesha mwanafunzi kuingizwa katika mchakato wa kutafutiwa sehemu ya field huhitajika kulipia gharama ya shilingi elfu ishirini. Kwa upande mwingine kujuana, undugu na rushwa hasa za mapenzi kwa akina dada imebainika kuwa ni siri ya kupata nafasi kwenye baadhi ya ofisi. Pia imegundulika kuwa sehemu nyingine huofia kuwalipa wanafunzi!!!

  Halikadhalika wanafunzi wametakiwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani utovu wa nidhamu imekua ni sababu nyingine pia ya wanafunzi kukosa nafasi za field. Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa moja ya vitu vinavyoongeza stress na ugumu katika maisha ya uanafunzi ni suala la field, hivyo wadau husika wa taasisi mbalimbali wanaombwa kufungua milango ya field kwani kufuatia ugumu huu imepelekea baadhi ya wanafunzi kutofanya kabisa field!!