Baada
ya kukaa kimya kwa miaka miwili, mwanamuziki wa miondoko ya Asili, Che
Mundugwao a.k.a Mtoto wa Lulindi ametoa nyimbo yake mpya inayoitwa KANDINDI.
Akizungumza na modreamz, Che Mundu
amesema KANDINDI, inazungumzia maisha yake halisi ya wakati akirudi nyumbani
kwao Lulindi Masasi na mchanganyiko wa
ladha ya asili na ladha ya mziki wa sasa (Bongo Beats). Ameongeza kuwa nyimbo
hiyo ameimba kwa lugha ya Kiyao kwani hata jina lenye lina maana ya ndege aitwae
Mdiria au King fisher kwa Kiingereza. Halikadhalika
Che Mundu amesema nyimbo hiyo itakata kiu ya mashabiki wake waliokua
wakimsubiri kwa muda mrefu.