Na Hilali Ruhundwa
Vyombo vya habari hapa
nchini vimetakiwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwa kutambua nafasi na
mchango wake katika kukuza demokrasia licha ya changamoto zilizopo. Hayo yamebainishwa na wataalam na wasomi
waliobobea katika taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mjadala kuhusu
ushiriki wa vyombo vya habari katika kutatua migogoro na kuimarisha amani (the
role of media in conflict resolution) pamoja na nafasi ya vyombo hivyo
katika demokrasia ya vyama vingi (Media Accountability in Tanzania’s
Multiparty Democracy) ulioandaliwa na hule uu ya uandishi wa habari na
mawasiliano kwa umma (School of Journalism and Mass Communication)
SJMC
|
Madam Zuhura Seleman |
Katika mhadhara huo
watoa mada walikuwa ni Dr. Ayoub Rioba aliyewasilisha mada kuhusu ushiriki wa
vyombo vya habari katika demokrasia ya vyama vingi Tanzania (Media
Accountability in Tanzania’s Multiparty Democracy) na Bi. Zuhura
Sulemani akitoa mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kutatua migogoro (The
role of media in conflict resolution).
Akiwasilisha mada Bi
Zuhura Selemain amesema kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vimekua kichocheo
cha migogoro mbalimbali ya kisiasa, kidini na kikabila barani Afrika akitoa
mfano wa mgogoro baada ya Uchanguzi(2007) nchini Kenya na mgogoro wa Burundi na
Rwanda. Akihitimsha mada yake Bi. Zuhura amesema vyombo vya habari sio chanzo
cha migogoro bali ni kichocheo cha migogoro iliyopo.
|
Dr Ayoub Rioba |
Kwa upande wake Dr Rioba amesema serikali
inawajibu wa kutambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari kwani vinauwezo
mkubwa wa kuitunza au kuharibu amani iliyopo Tanzania.
Mhadhara huo
ulihudhuriwa na wadau mbalimbali katika sekta ya habari na mawasiliano nchini akiwamo Bw. Samwilu Mwafisi
aliyekua Mkurugenzi wa TUT( Taasisi ya Utangazaji Tanzania) kwa sasa ni TB, Mama
Eda Sanga ambaye ni Meneja Uzalishaji,Mlimani Media Said Kubenea na Bw Mbwilo
Kitujme Mhariri wa Habari TBC.