Nikiwa katika mihangaiko ya kazi nikaenda kwenye ofisi moja maeneo ya Ubungo. Nilipokelewa na mama mmoja (mlinzi) wakati ananipa utaratibu nilikuwa na mshangaa kwa masikitiko kwa jinsi alivyoharibika uso wake (kaungua na kuweka ukungu mweusi). Kwa nyakati hizi imekuwa kawaida kukutana na watu wa aina hii wengine utawakuta ni weupe kupitiliza, wengine wekundu, wengine wamebabuka yaani balaa tupu! sio tu akina dada bali hata akina kaka nao wamejiingiza katika matumizi ya Creams.
Moja ya wanawake walioharibika kutokana na matumizi ya vipodozi pic by modernghana |
Creams ninazozitahaja hapa ni lightening (bleaching) creams ambazo zime-contain mercury and hydroquinone, alpha hydroxyl acids, Arsenic,na nyinginezo nyingi.Kutokana na utafiti wa Dr S Allen Counter 2003 ilionekana kuwa sumu ya mercury (zebaki) imekutwa kwenye miili ya watu wengi wao wakiwa wanawake. Nchi zilizooneka kuwa vinara katika hili ni Mexico,Saudi Arabia, Senegal,Tanzania na nchi nyingine za Afrika magharibi. Sababu kubwa unayowafanya watu kuji-cream (kujichubua) ni kwa ajili kwa kutaka kuonekana warembo. Lakini hii ni kasumba mbaya kwani kuwa mrembo au kuonekana unapendeza ni lazima uwe mweupe? HAPANA tena tafiti zinaonyesha kuwa most beautiful and attractive women in the world are actually black women! Angalia akina Naomi Campbell, Halle Berry, Tyra Banks,Miriam Odemba, Nancy Sumari na wengine wengi. Kibaya zaidi tunaambiwa “Beauty is more than skin deep” . Athari kubwa zimekuwa zikionekana sana huku kwetu Afrika kwa sababu vipodozi hivi vingi haviko favorable na mazingira yetu kwani watngenezaji wanashauri watumiaji wasiwe wanakaa jua au watumie sunblock masharti haya wengi wa akina dada zetu yamewashinda!! Hivyo kujikuta wanababuka ngozi zao, athari nyingine ambazo zinazowatokea ni kuzeeka kwa ngozi kutokana na mikunjo hivyo kumfanya kijana anaonekane mzee, kupata cancer hali kadhalika kifo chaweza kutokea kwa wale wanaofanya plastic surgery.
Nancy Sumari one of the black beautiful girl |
Licha ya vipodozi hivi kupigwa marufuku katika nchi mbalimbali lakin bado vimekuwa vikiuzwa kinyemela.Imeshauriwa kuwa watumiaji waepuke vipodozi vyenye chemical hizo au watumie vipodozi vya asili (HERBAL) ambavyo vinaweza kulinda urembo wao.
Jikubali ulivyo because you are beautiful in your natural color.