Safari ni safari

Vijana wa Kijiji cha Nkuhi Kata ya Isuna, Mkoa wa Singida, wakisafiri kwa baiskeli huku mmoja wao akiwa amelala katika mwamba, hali hilo inatokana na shida ya usafiri katika eneo hilo. (Picha na Prona Mumwi/MAJIRA)
Picha na wavuti.com

Wale ambao hamjahesabiwa sensa..toa taarifa kwa namba hizi...

-- Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeongeza mbele tarehe za kumaliza kazi ya Sensa ya Watu na Makazi hadi Jumamosi ya tarehe 8 Septemba mwaka huu ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliyebaki anahesabiwa. Hivyo wito umetolewa kwa mwananchi hawajafikiwa na Makarani wa Sensa watoe taarifa katika Ofisi za Serikali za Mitaa au Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuhesabiwa. Kamishna wa Sensa kutoka NBS Hajjat Amina Mrisho ametoa  wito kwa wale ambao hawajaandikishwa hadi hivi sasa kuwa wanatakiwa watume taarifa kwa namba 2122724, 0754583415, 2129622 , 0713335429, 0713574622 na 0713312699