Our time to say Goodbye

    Jana was happy, great and unforgettable day to all Jitegemee form four students because they were saying kwaheri (graduating) kwa walimu na wanafunzi wenzao  walioishi nao kwa miaka minne hapo shuleni kwao.
Baadhi ya wanafuzi wakiwa katika pozi
Mdau Edo (kushoto) ni mmoja wa wahitimu
Wote walikuwa na furaha huku wakionesha  hamu ya kuingia kidato cha tano.

Poziiiiii!!
     Sherehe hiyo ilifanyika shule hapo maeneo ya Kurasini kilwa road,kulikuwa na burudani zilizotolewa na wanafunzi wenyewe na vituko kama kawaida havikukosekana.
Mshikaji akihuzunika kwa kumaliza chakula chake!!
Big aking'ang'ana na kipapatio cha kuku!!
  Wanafunzi wote wamefurahia kuhitimu elimu ya sekondari na wanaomba uzima na nguvu ilikufika tarehe 3 october na waweze kufanya mitihani yao salama. Pia wameshukuru kwa sherehe hiyo kufanyika kabla ya mitihani kwasababu itawasaidia kupunguza stress na hofu ya mtihani.
May GOD BE WITH YOU ALL FORM FOUR STUDENTS & ALL THE BEST KATIKA MITIHANI YENU HAPO TAREHE 3.

MAOMBOLEZO TANZANIA

Kufuatia msiba ulioikumba Tanzania kutokana na ajali ya boti ya MV Spice Islander iliyotokea katika eneo la Nungwi katikati ya bahari ya Hindi, Serikali  imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo tarehe 11,hivyo bendera itapepea nusu mlingoti kuashiria maombolezo hayo. Halikadhalika serikali imeridhia kuzika miili ya maiti zote ambazo hazitatambulika. Kutokana na ajali hiyo,imethibitika  takribani watu 192 na wengine zaidi ya 600 wameokolewa.  Taarifa za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kubeba  abiria na mizigo  mingi zaidi ya uwezo wake. Kwa upande wao jeshi la Polisi nchi limeunda  za uokoaji wa majeruhi na kuchunguza  chanzo cha ajali hiyo.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakitoa heshima kwa marehemu.

Rais Kikwete akiangalia miili ya vichanga waliofariki katika ajali hiyo.
Miili ya marehemu ikisuburi kutambuliwa na ndugu zao


Hii ni ajali kubwa ya kwanza kutokea katika mwambao wa Zanzibar. Modreamz inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu MUNGU AZILAZE  ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.

                                                                                                                         pic from jikumbuke blog

Salha Israel,the new Miss Tanzania 2011.

   Shindano la Vodacom Miss Tanzania limemalizika kwa Salha Israel kuibuka mshindi na kutwaa taji hilo kwa mwaka 2011.Washindi wengine ni Tracy Sospeter kutoka Shinyanga aliyeshika nafasi ya pili na Alexia William kutoka Kinondoni aliyepata nafasi ya tatu.
Miss Tanzania 2011 Salha Israel (katikati) akiwa na washindi wengine Tracy Sospeter (kulia) na Alexia William (kushoto)
Kufuatia ushindi huo Salha ataiwakilisha Tanzania katika shindano la urembo duniani ( Miss World 2011).All THE BEST n TAKE CARE COZ EVERY EYES ARE ON YOU.
Salha Israel Miss Tanzania 2011 akivishwa taji lake

You are beautiful in your color!!

Nikiwa katika mihangaiko ya kazi nikaenda kwenye ofisi moja maeneo ya Ubungo. Nilipokelewa na mama mmoja (mlinzi) wakati ananipa utaratibu nilikuwa na mshangaa kwa masikitiko kwa jinsi alivyoharibika uso wake (kaungua na kuweka ukungu mweusi). Kwa nyakati hizi imekuwa kawaida kukutana na watu wa aina hii wengine utawakuta ni weupe kupitiliza, wengine wekundu, wengine wamebabuka yaani balaa tupu! sio tu akina dada bali hata akina kaka nao wamejiingiza katika matumizi ya Creams.
Moja ya wanawake walioharibika kutokana na matumizi ya vipodozi pic by modernghana

      Creams ninazozitahaja hapa ni lightening (bleaching) creams ambazo zime-contain mercury and hydroquinone, alpha hydroxyl acids, Arsenic,na nyinginezo nyingi.Kutokana na utafiti wa Dr S Allen Counter 2003 ilionekana kuwa sumu ya mercury (zebaki) imekutwa kwenye miili ya watu wengi wao wakiwa wanawake. Nchi zilizooneka kuwa vinara katika hili ni Mexico,Saudi Arabia, Senegal,Tanzania na nchi nyingine za Afrika magharibi. Sababu kubwa unayowafanya watu kuji-cream (kujichubua) ni kwa ajili kwa kutaka kuonekana warembo. Lakini hii ni kasumba mbaya kwani kuwa mrembo au kuonekana unapendeza ni lazima uwe mweupe? HAPANA tena tafiti zinaonyesha kuwa most beautiful and attractive women in the world are actually black women! Angalia akina Naomi Campbell, Halle Berry, Tyra Banks,Miriam Odemba, Nancy Sumari na wengine wengi. Kibaya zaidi tunaambiwa “Beauty is more than skin deep” . Athari kubwa zimekuwa zikionekana sana huku kwetu Afrika kwa sababu vipodozi hivi vingi haviko favorable na mazingira yetu kwani watngenezaji wanashauri watumiaji wasiwe wanakaa jua au watumie sunblock masharti haya wengi wa akina dada zetu yamewashinda!! Hivyo kujikuta wanababuka ngozi zao,  athari nyingine ambazo zinazowatokea ni kuzeeka kwa ngozi kutokana na mikunjo hivyo kumfanya kijana anaonekane mzee, kupata cancer hali kadhalika kifo chaweza kutokea kwa wale wanaofanya  plastic surgery.
Nancy Sumari one of the black beautiful girl
  Licha ya vipodozi hivi kupigwa marufuku katika nchi mbalimbali lakin bado vimekuwa vikiuzwa  kinyemela.Imeshauriwa kuwa watumiaji waepuke vipodozi vyenye chemical hizo au watumie vipodozi vya asili (HERBAL) ambavyo vinaweza kulinda urembo wao.
Jikubali ulivyo because you are beautiful in your natural color.

VOTE FOR Mt KILIMANJARO


   Ukiwa kama mdau wa unahimizwa kuuwezesha mlima Kilimanjaro kushinda na kuwa moja ya maajabu ya dunia. Hii ni kupitia shindano la new 7 world wonders linaloendeshwa hivi sasa. Mlima Kilimanjaro una mita 5895 kutoka usawa wa bahari  (5895 from the sea level)  una vigezo vyote vya kuingia katika  new world wonders, kwanza   kabisa ni mlima mrefu kuliko yote barani Africa, pia una vilele viwili ambavyo ni Kibo na Mawenzi zaidi ni kwamba, inastaajabisha kwa mlima kama huu (Volcanic mountain)  kuweko katika ukanda wenye hali ya hewa ya Kitropiki.
 Kuupigia kura ni rahisi tembelea www.new7wonders.com au bofya  hapahttp://www.new7wonders.com/vote-2?lang=en
      Lets unite & enable mount Kilimanjaro to be the new world wonder.