MAOMBOLEZO TANZANIA

Kufuatia msiba ulioikumba Tanzania kutokana na ajali ya boti ya MV Spice Islander iliyotokea katika eneo la Nungwi katikati ya bahari ya Hindi, Serikali  imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo tarehe 11,hivyo bendera itapepea nusu mlingoti kuashiria maombolezo hayo. Halikadhalika serikali imeridhia kuzika miili ya maiti zote ambazo hazitatambulika. Kutokana na ajali hiyo,imethibitika  takribani watu 192 na wengine zaidi ya 600 wameokolewa.  Taarifa za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kubeba  abiria na mizigo  mingi zaidi ya uwezo wake. Kwa upande wao jeshi la Polisi nchi limeunda  za uokoaji wa majeruhi na kuchunguza  chanzo cha ajali hiyo.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakitoa heshima kwa marehemu.

Rais Kikwete akiangalia miili ya vichanga waliofariki katika ajali hiyo.
Miili ya marehemu ikisuburi kutambuliwa na ndugu zao


Hii ni ajali kubwa ya kwanza kutokea katika mwambao wa Zanzibar. Modreamz inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu MUNGU AZILAZE  ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.

                                                                                                                         pic from jikumbuke blog

No comments: