Atoka Mbeya mpaka Dar es Salaam kwa baiskeli

Katika hali ambayo humkuta kila mwanadamu kutaka kutumia kipaji chake ili kujipatia kipato binafsi, kijana John Mwaipaya kutoka Songwe jiji Mbeya amechukua maaumuzi ya kuja jiji Dar es Salaam kuendeleza michezo yake ya baiskeli. Anasema kilichomfanya aje jijini Dar, baada ya kutopata mafanikio jiji Mbeya kupitia mchezo huo, hivyo amekuja Dar kutafuta wafadhili watakao msaidia kukuza na kuendeleza kipaji chake cha michezo ya baiskeli. "Mbeya kazi ilikua ngumu sana, yaani nimejitahidi kutunga michezo mingi na kuionyesha lakini hakuna mtu anayeithamini,hivyo nilisikia Dar kuna watu wanaoweza kunisaidia kuendeleza michezo yangu" amesema John.

Michezo hii,nimeigundua mwenye,hakuna aliyenifundisha na nimeifanya kwa muda wa miaka nane sasa aliongeza bwana John.
Anasema alipofika Dar amekuta mambo ni tofauti na alivyofikiri kwani imekua ni ngumu kupata mtu wa kuendeleza kipaji hicho. Nilipofika Dar, nilifikia Ukonga kwa shemeji yangu, lakini kwa niliondoka baada ya muda mfupi kutoka ungumu pale nyumbani kwa sasa  nipo Magomeni amesema bwana John.
Halidhalika bwana John amesema anafanya shughuli hiyo kwa kuzunguka sehemu mbalimbali na kuonyesha michezo hiyo."Huwa watu wanajikusanya kila mwenye kiasi chochote hutoa halafu ndo naanza kuonyesha" amesema bwana John. Ninachokipata ni kiasi kinachoniwezesha kupata hela ya kula tu.

Bwana John ana ndoto za kufungua chuo kitakachowafundisha vijana michezo mbalimbali ya baiskeli. Hivyo kufanya fani hiyo kuwa sehemu itakayowawezesha vijana kujipatia ajira rasmi.


No comments: