HII INA KUHUSU MTUMIAJI WA INTERNET!!

  Katika dunia ya sasa suala mifumo ya upokeaji wa taarifa  na mawasiliano (information and communication technology-ICT) kwa sasa limekua sana, sio tu kwa nchi zilizoendelea hata kwa nchi zinazoendelea mfano mzuri ni hapa nyumbani Tanzania,tumeona kwa kiasi chake maendeleo ya mifumo ya digitali na satelaiti( digital & satelite),na intanet vikiongezeka kwa kasi.Chakusikitisha ni kwamba badala ya maendeleo haya kutusaidia kusonga mbele,sasa yamegeuka kikwazo cha sisi kufikia maendeleo yanayohitajika kwa mfano uwepo wa intaneti sio  tu kwa kutuvunjia maadili bali hata kwa kutupotezea muda mwingi wa kufanya shughuli nyingi za kimaendeleo.Kwani hivi sasa watu hutumia muda mwingi ku-chat kwenye facebook au twitter.Kibaya zaidi kinachozungumzwa humo ndani ni upuuzi usiojenga.

Jamaa kakomaa na surakitabu       (pic wavuti.com)
    Kwa wenzetu vitu vinawasaidia sana sio tu katika mawasiliano bali hata kutangaza biashara zao,katika elimu (online education) na zaidi hata kutoa nafasi za ajira.Tofauti kabisa na hapa kwetu,bado tuna ile kasumba ya kizamani ya kuhisi kuwa facebook ipo kwa ajili ku-upload picha tu.Unaweza kukuta mtu amekesha internet lakini anachokifanya hakina manufaa.Imefika wakati tubadilishe mitazamo yetu,tutumie vyombo hivi kwa namna itakayotuletea manufaa.