Waandaaji Wema VS Wolper lawamani!!


Katika kulizungumzia tamasha la Matumaini lililofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita, moja ya vitu vilivyowavuta wengi ni pambano la ngumi kati ya Wema Sepetu na Jackline Wolper, kwa sababu ilikua ni kitu cha tofauti kutokea kwa hapa kwetu….kuwapambanisha wasanii maarufu ambao sio mabondia. Kwa hakika ilikua ni kitu kilichoongeza msisimko kabla ya tamasha kuanza kwa sababu kila mmoja alitaka kuona wadada hao wakitoana manundu.
Cha kusikitisha kinyume na matarajio ya wengi pambano lile halikua na mvuto kama ilivyotegewa, kwani hakuna ngumi zilizorushwa zaidi ya Wema na Wolper kurukaruka ulingoni, kuchekacheka na kushikanashikana kusipokua na sababu na mwishowe kuwachosha mashabiki na kuwafanya kutoa lawama zao katika vyombo vya habari na mtandaoni.
Hebu tujiulize  Wema na Wolper si waigizaji wa filamu??hivi walishindwa kabisa kuigiza kama wanapigana kweli??Hapana kwa hakika wanauwezo wa kufanya hivyo,ila uzembe na lawama zote zinaenda kwa waandaaji wa mpambano ule kwa kushindwa kujipanga na kukosa ubunifu…..
Ubunifu ulikosekana ilikua katika uandishi wa script (mwongozo) wa kusimamia pambano lile au kama script ilikuepo basi alieandika hakujua  nini cha kufanya…..kwani script yake ilishindwa kuwafanya Wema na Wolper wapigane kiuongo na kweli, iilshindwa hata kuwafanya warushe makonde na kuwatoa kijasho mfano ukiangalia vizuri ile sehemu Wema aliyokimbia na kwenda kumkumbatia refa ilikua ni nzuri lakini ya kijinga kwa sababu Wolper hakurusha ngumi ambayo ingemfanya Wema akimbie…hata kama walikua wanaogopa kuumizana basi script ilitakiwa iwaongoze sehemu za kupigana mfano mikononi n.k…...kwa kufika mbali zaidi script ingetakiwa hata itoe mshindi mmoja ili baadae hata waweze kuandaa pambano la marudiano ambalo lingewawezesha kupata fedha nyingi zaidi na kufanikisha ujenzi wa mabweni ya wasichana kama ilivodhamiriwa

Hakika tulichokiona ilikua ni kuchoshana kwa ufupi Wema na Wolper hawakupigna waandaji walitakiwa kuonesha pambano la  ukweli ….mfano mzuri  wrestling (mieleka) mapambano mengi yanaongozwa na script na  mshindi anapangwa lakini bado wapiganaji wanapigana kiukweli..hii ni kwa sababu lengo linakua ni kutoa burudani kwa watazamaji.