Katika kulizungumzia tamasha la Matumaini
lililofanyika Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita, moja ya vitu vilivyowavuta
wengi ni pambano la ngumi kati ya Wema Sepetu na Jackline Wolper, kwa sababu
ilikua ni kitu cha tofauti kutokea kwa hapa kwetu….kuwapambanisha wasanii maarufu ambao sio mabondia. Kwa hakika
ilikua ni kitu kilichoongeza msisimko kabla ya tamasha kuanza kwa sababu kila
mmoja alitaka kuona wadada hao wakitoana manundu.
Cha kusikitisha kinyume na matarajio ya
wengi pambano lile halikua na mvuto kama ilivyotegewa, kwani hakuna ngumi
zilizorushwa zaidi ya Wema na Wolper kurukaruka
ulingoni, kuchekacheka na kushikanashikana
kusipokua na sababu na mwishowe kuwachosha mashabiki na kuwafanya kutoa lawama
zao katika vyombo vya habari na mtandaoni.
Hebu tujiulize Wema na Wolper si waigizaji wa filamu??hivi
walishindwa kabisa kuigiza kama wanapigana kweli??Hapana kwa hakika wanauwezo
wa kufanya hivyo,ila uzembe na lawama zote zinaenda kwa waandaaji wa mpambano
ule kwa kushindwa kujipanga na kukosa ubunifu…..
Ubunifu
ulikosekana ilikua katika uandishi wa script
(mwongozo) wa kusimamia pambano lile au kama script ilikuepo basi alieandika hakujua nini cha kufanya…..kwani script yake ilishindwa kuwafanya Wema na Wolper wapigane kiuongo na kweli, iilshindwa hata kuwafanya
warushe makonde na kuwatoa kijasho mfano ukiangalia vizuri ile sehemu Wema
aliyokimbia na kwenda kumkumbatia refa ilikua ni nzuri lakini ya kijinga kwa
sababu Wolper hakurusha ngumi ambayo ingemfanya Wema akimbie…hata kama walikua
wanaogopa kuumizana basi script
ilitakiwa iwaongoze sehemu za kupigana mfano mikononi n.k…...kwa kufika mbali
zaidi script ingetakiwa hata itoe
mshindi mmoja ili baadae hata waweze kuandaa pambano la marudiano ambalo
lingewawezesha kupata fedha nyingi zaidi na kufanikisha ujenzi wa mabweni ya
wasichana kama ilivodhamiriwa
Hakika tulichokiona ilikua ni kuchoshana kwa ufupi Wema na Wolper hawakupigna waandaji walitakiwa kuonesha pambano la ukweli ….mfano mzuri wrestling (mieleka) mapambano
mengi yanaongozwa na script na mshindi
anapangwa lakini bado wapiganaji wanapigana kiukweli..hii ni kwa sababu lengo
linakua ni kutoa burudani kwa watazamaji.
No comments:
Post a Comment