PICHA YA WATOA KIMAISHA!!

Kwa miaka 11, Rozonno na mkewe Mia McGhee walifanya kila walichokiweza ili waweze kuzaa mtoto angalau mmoja,hatimaye mwaka jana mwezi juni Mia alifanikiwa kupata mimba na kujifungua si mtoto mmoja bali watoto mapacha sita

Lakini mahitaji ya watoto hao wachanga yalikuwa makubwa kuliko uwezo wao. Kwa siku watoto hao walitumia jumla ya nepi 50 na chupa 30 za maziwa
Mia alimwambia mumewe waweke pozi na watoto wao na walipiga picha ambayo Mia aliiweka kwenye mtandao wa Facebook kwani maombi yao ya msaada kwa manispaa yalikataliwa.

Picha hiyo ilijipatia umaarufu duniani na haikuchukua muda ilimfikia bilionea Oprah Winfrey ambaye alivutiwa na picha hiyo na kuamua kumualika Rozonno na mkewe kwenye shoo yake pia Oprah aliizawadia familia hiyo dola 250,000 za kufanya manunuzi ya mahitaji yao yote wakati wowote wanapotaka kwenye mtandao wa supermarket kubwa Marekani ya Walmart.

Ingawa Rozonno na mkewe walishaoana miaka 11 iliyopita walipokuwa na umri wa miaka 18 na 19, Oprah aliwazadia zawadi ya kwenda fungate (honeymoon) kwenye mojawapo ya hoteli kubwa za mjini Las Vegas.

KUDUME CHA DUNIA.

Huyo si mwingine bali ni mzee Ziona Chana mwenye  miaka 67 ambaye pamoja na kuwa na wake 39, watoto 94, wajukuu 33 lakini bado ana mpango wa kuongeza wake wengine zaidi ili kuikuza familia yake.Familia nzima ina watu 181 inaishi kwenye nyumba moja kubwa ya ghorofa nne yenye  vyumba 100 iliyopo katika kijiji cha Baktwang katika jimbo la Mizoram nchini India.

Msosi wa usiku mmoja pekee unapoandaliwa ni sawa na maandalizi ya sherehe fulani kwani jumla ya kuku 39, kilo 60 za viazi na kilo 100 za mchele hutumika ili kuitosheleza familia nzima kwa usiku mmoja tu achilia mbali chakula cha mchana na brekfasti


Mwenyewe ajigamba kuwa mwanaume mwenye bahati kwa kumiliki   wake 39 na kuwa mkuu wa familia kubwa kuliko zote duniani.

       Mjengo wa mzee Ziona ambapo anaishi na familia yake

Hiki ni chumba za wake zake kwani yeye huishi kwenye chumba cha peke yake  ambapo wake zake 39 hupeana zamu za kulala ndani ya chumba hicho na mzee huyo wa kaya.