DARUSO SJMC & MCT PANEL DISCUSSION, YAFANA


Uongozi wa serikali ya wanafunzi katika Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano kwa Umma ikishirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT), imefanya mhadhara  wenye lengo la kujadili na kuwanoa  waandishi wa habari chipukizi (nurturing upcoming professionals)  ulikua na lengoi suala la maadili katika taaluma ya uandishi wa habari. Katika  uaslishaji wa mada yake Bwana Chrisosto Rweyemamu alisisitiza kuwa kwa waandishi wa habari chipukizi wana  wajibu wa kusoma na kuuelewa Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji kwani ndio dira na nguzo ya tansia ya habari nchini.
 
Kwa upande wake mwanahabari mwandamizi,Madam Rose amesema ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya uandishi wa habari huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu mikataba ya ajira miongoni mwa mwaandishi wa habari. Hivyo kuwafanya waandishi wengi kudanganyika kwa ‘brown envelope’ maarufu kama “mshiko” kwa kuwa hawana job security.
Katika kuhitimsha mhadhara huo Dean wa shule kuu ya habari ya mawasiliano kwa umma Dr Herbert Makoye amepongeza jitihada zilizonyeshwa na DARUSO SJMC kwa kuandaa mihandara yenye lengo la kupanua fikra za wanafunzi .
Ngwegwe Mussa mwenyekiti wa DARUSO SJMC

Dr Hebert Makoye akimkaribisha mgeni rasmi
Madam Rose akiwasilisha mada yake.

Prof Tompson alitoa pia uzoefu wake kutoka nchini Marekani
Umati uliohudhuria mhadhara huo

Mzee Mrutu




Wadau wakifuatilia mhadhara