HATUWEZI KUENDELEA KWA NCHI ILIYOJAA WANYOA VIDUKU!!

  Nafurahishwa sana kwa kuona muamko mkubwa wa Watanzania wengi  kutaka kuwa na maendeleo katika nchi yetu, hamasa hii inatokana  na kufunguka kifikra na kiakili miongoni mwa watu hivyo kupelekea kujitambua na kujua haki zao na kipi wa wanachokitaka  kiwepo katika jamii yetu. Lakini kwa masikitiko makubwa napenda kuwa vunja moyo kwa kuwaambia kuwa HATUWEZI kupata maendeleo kwa taifa lililojaa wanyoa viduku na wavaa supra!!” .   Najua unajiuliza kwani kuvaa supra na konyoa kiduku  kuna mahusiano gani na suala la maendeleo?? Sina  maana ya wazi kiiivo ,naamanisha kuwa suala la maendeleo hushangiwa kwa kiasi  kikubwa na kupevuka kwa fikra kwani hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa” Umasikini wa fikra ni umasikini mkali kuliko yote” lakini wengi wetu hasa vijana bado hatujataka  kuzipevua akili zetu bali tumezidi kuzidumaza fikra zetu kwa kufikiria kunyoa viduku,kuvaa  kata K, huku tuikimba Muhogo andazi, Muhogo andazi, na kwa sauti kubwa tunaimba ni sababu ya Ulofa na nyimbo nyingine za mahadhi hayo. Zaidi ya hapo tunafikiria ni lini tutaenda kupiga picha za editing kule my fair au photo point! Kubali kataa hayo ndio mawazo ya sisi vijana wa leo. Mfano mzuri ni wengi wa wanamuziki wetu vijana hawatoi nyimbo zenye hamasa kwetu.
  Tunapozidi kujilemaza namna hiyo tunawapa wazee wajanja mianya ya kupiga chada ( fedha) na kutuacha tukilalama bila msingi huku wakitulipa fadhila kwa kutuuzia hiyo midosho ya supra waliyoagiza kutoka China. Najua wapo watakosema kuwa tunaenda na fashion! Hata kama ndiyo, bali tujaribu kubadilisha mitazamo yetu kwani hata nchi zilizokuwa   masikini zikaendelea (India na Indonesia) walianza kubadilisha fikra kwanza,  walikuwa wakifikiria na kuzungumza mageuzi katika kila jambo na hata ilipowezekana kucheka au kutembea basi walifanya hivyo kwa namna ya kimapinduzi. Nasi tuige mambo hayo.  Kama vijana tuamke, tuone,tusimame, tusome,tujifunze ili tufunguke kifikra. Nazungumzia sana fikra kwa sababu ndiyo kipimo sahihi cha mtu kuelimika sio lazima wote tupate ‘A’ darasani bali kusoma maandiko makini ndio yatakayofungua akili zetu.(make us conscious). Ukiangalia kwa nchi za wenzetu vijana tena wenye miaka kati ya 20 mapaka 35 ndio manaofanya mageuzi makubwa ya kimaendeleo hii ni kwa sababu wamejengewa misingi ya kujitambua na kujiendeleza  lakini natambua kwa hapa kwetu mifumo ya maisha bado haituwezeshi vijana kufikia malengo yetu, lakini hiyo sio kikwazo cha kutufanya sisi tumbweteke!
  Tumeshaambiwa kuwa vijana sio tena taifa la kesho bali ni Taifa la leo,hivyo hatuna budi kuchagua mfumo sahihi wa maisha yetu. 

2 comments:

NellyNice said...

sawasawa kaka nimekupata mkuu

Anonymous said...

conscious ndo mpango mzima mdau TANZANIA BILA VIDUKU INAWEZEKANA