UHURU WA HABARI TANZANIA #Hekaya za Ray Mtani
Na Raymond Mtani
Leo ni siku ya uhuru wa habari dudiniani, lengo kuu la maadhimisho ya siku hii may 3, (world press freedom day) ni:
• kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa uhuru wa habari na
• kukumbusha serikari wajibu wake wa kuheshimu na kuthamini haki ya
uhuru wa kujieleza kama unavyotajwa katika Ibara ya 19 ya mkataba wa
haki za binadam.
Labda kwa faida ya jumla Ibara ya 19 ya
mkataba wa kimataifa wa haki za binaadam inasomeka hivi “Everyone has
the right to freedom of opinion and expression; the right includes
freedom to hold opinions without interference and to seek, receive and
impart information and ideas through any media regardless of frontiers”
Kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki
ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila kujali mipaka. Zaidi tafsiri
ya Ibara hiyo imehuishwa katika ibara ya 18 ya katiba ya JMT 1977 na
mabadiliko yake ya mwaka 2005.
Kwangu mimi siku hiyo ni zaidi ya
muhimu kwa ustawi wa demeokrasia ya nchi yetu, ni muhimu kwa ajili ya
kuhamasisha na kuchochea mawazo mbadala, hasa ikizingatiwa kuwa mwaka
huu waandishi na jamii ya wapenda haki za binadamu wanaadhimisha siku
hiyo kukiwa na kumbukumbu ya matukio mabaya kupata kutokea katika
historia ya nchi yetu,
Naam nitataja machache, mosi ni mauaji
ya kinyama ya mwandishi Daudi mwangosi akiwa kazi kutafuta habari kama
ibara ya 18,(b) ya katiba ya JMT inavyompa haki hiyo. Ipo kumbukumbu ya
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri kutekwa, kuteswa, kung’olewa kucha,
jicho na kasha kutelekezwa hadi leo hii yungali anauguza majeraha huko
Afrika kusini.
Vile vile tunaadhimisha siku hiyo kukiwa na
kumbukumbu ya kutekwa, kuteswa, kungolewa kucha, meno na kutelekezwa
katika msitu wa Pande kwa mwanyekiti wa jumuhiya ya mdaktari nchini Dr
steven Olimboka, huyu alikuwa katika harakati za kukuza uhuru wa
kujileza(haki ya msingi ya kikatiba)
Kama hiyo haitoshi ni hivi
juzi may 1, mkuu wa mkoa wa Arusha alitishia waandishi wa habari
akiwataka kuwa makini pindi wanapoandika habari zinazohusu migogoro ya
viongozi akienda mbali zaidi na kudai roho zao zitakua mkononi
"Unapoingia katika mkakati wa kudhalilisha kiongozi wa serikali unakuwa
umeiweka roho yako rehani, kuweni makini" alisema Magesa Mulongo mkuu
wa mkoa wa Arusha katika maadhimisho ya siku ya wafanya kazi duniani.
Tunaadhimisha siku hii kukiwa na jaribio la Bunge kuzuia vyombo vya
habari kurusha matangazo yake ya moja kwa moja ingawa jaribio hilo
linaonekana kushidwa juhudi zingali zinafanywa hii ni kutokana na
kiongozi mkuu wa bunge Speaker Anne Makinda kurudia mara kwa mara kuwa
hawafanyi kazi taarifa za vyombo vya habari.
Mbali na msululu
wa sharia mbovu zinazonyima waandishi na vyombo vya habari kwa ujumla
kufanya kazi zao kwa weledi kwa kutoa taarifa zenye ushahidi wa kina,
serikali imekuwa ikitumia lungu la sharia hizo mbovu kushitaki
waandishi na kufungia kila chombo cha habari kinachokinzana na matakwa
yake, wote tunakumbuka tukio la kufungiwa kwa gazeti la MWANAHALISI.
Orodha ni ndefu sana, yatosha kusema kila mtanzania kwa nafasi yake
anawajibika kushinikiza serikali hii kuheshimu uhuru wa habari,
kujieleza ni haki pekee ya msingi, siyo matakwa ya mtu bila kuwa makini
kupitia haki hii tutaibiwa, tutanyanyaswa, tutateswa na kufanyiwa kila
hila.
Namaliza kwa kusema ni rahisi sana kumuua mtu kuliko kumyamazisha kusema.
No comments:
Post a Comment