SJMC PUBLIC LECTURE YAFANA

Na Hilali Ruhundwa


Vyombo vya habari hapa nchini vimetakiwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwa kutambua nafasi na mchango wake katika kukuza demokrasia licha ya changamoto zilizopo.  Hayo yamebainishwa na wataalam na wasomi waliobobea katika taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mjadala kuhusu ushiriki wa vyombo vya habari katika kutatua migogoro na kuimarisha amani (the role of media in conflict resolution) pamoja na nafasi ya vyombo hivyo katika demokrasia ya vyama vingi (Media Accountability in Tanzania’s Multiparty Democracy) ulioandaliwa na hule uu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (School of Journalism and Mass Communication) SJMC

Madam Zuhura Seleman
Katika mhadhara huo watoa mada walikuwa ni Dr. Ayoub Rioba aliyewasilisha mada kuhusu ushiriki wa vyombo vya habari katika demokrasia ya vyama vingi Tanzania (Media Accountability in Tanzania’s Multiparty Democracy) na Bi. Zuhura Sulemani akitoa mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kutatua migogoro (The role of media in conflict resolution).

Akiwasilisha mada Bi Zuhura Selemain amesema kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vimekua kichocheo cha migogoro mbalimbali ya kisiasa, kidini na kikabila barani Afrika akitoa mfano wa mgogoro baada ya Uchanguzi(2007) nchini Kenya na mgogoro wa Burundi na Rwanda. Akihitimsha mada yake Bi. Zuhura amesema vyombo vya habari sio chanzo cha migogoro bali ni kichocheo cha migogoro iliyopo.


Dr Ayoub Rioba
 Kwa upande wake Dr Rioba amesema serikali inawajibu wa kutambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari kwani vinauwezo mkubwa wa kuitunza au kuharibu amani iliyopo Tanzania.
Mhadhara huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali katika sekta ya habari na  mawasiliano nchini akiwamo Bw. Samwilu Mwafisi aliyekua Mkurugenzi wa TUT( Taasisi ya Utangazaji Tanzania) kwa sasa ni TB, Mama Eda Sanga ambaye ni Meneja Uzalishaji,Mlimani Media Said Kubenea na Bw Mbwilo Kitujme Mhariri wa Habari TBC.


No comments: