HII NDIYO AFRIKA YETU.

    Naamini bara la Afrika ni moja ya sehemu iliyobarikiwa sio tu kwa rasilimali zilizopo bali pia kuwa na watu wenye nguvu kuliko sehemu nyingine duniani. Lakini cha ajabu ndio sehemu inayoongoza  kwa matatizo kama vita (vurugu),ufukara,ufisadi,njaa na ukame kuliko sehemu  yoyote.Sijui tatizo letu ni nini??. Wapo wanaosema eti WAAFRIKA TUMELAANIWA!! Mimi siamini kwamba tumelaaniwa kwani Mungu hawezi kuwa katili na muonevu kwa Waafrika kiasi hicho,tatizo lipo sehemu limejificha,kuzungumzia LAANA ni uvivu wa kufikiri  na uwoga wa kuumiza kichwa katika ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili.


    Kwa upande mwingine inaniingia akilini kwamba yaweza kuwa laana,tena iliyotoka kwa shetani, hii inatokana na matendo yatunayofanya waafrika. Mfano mzuri ni hali inayoendelea huko pembezoni mwa afrika katika nchi ya Somalia,kwa muda wa miezi mine sasa imekumbwa na ukame na njaa illiyosabisha njaa kali kwa wananchi na mifugo yao. Hali hii imesababisha vifo vya mamia ya watu hasa watoto na wengine maelfu kukimbilia nchi za Kenya na Ethiopia kama wakimbizi.

Baadhi ya wakazi wa Somalia waliokimbilia Kenya
   
 Kutokana na hali hii mashirika ya kibinadamu kama Save the children wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwa wakimbizi kwa wananchi wa Somalia na wamekuwa wakitoa taarifa kuwa hali inazidi kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba wafanyakazi wa shirika hili wamekuwa wakivamiwa na waasi hivyo kukwamisha zoezi la utoaji wa misaada. Hata baada ya umoja wa maataifa kupitia shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mradi wa chakula duniani (World Food Programe) kuamua kwenda kutoa  misaada ya chakula,waasi hawa wa Alshabab wameanzisha mapigano makali dhidi ya mashirika haya,huko mjini Mogadishu.

Mama wakisomali akiwa na mwanae
   Hakika huu ni ukatili wa hali ya juu,licha ya kuona wenzao(ndugu zao) wanasulubika kwa tatizo la njaa bado wameamua kuwazuia kupata chakula hicho. Nahisi lengo lao ni kuwamaliza kabisa.Kwanini waafrika tumekosa utu na huruma kwa wenzetu? Kwa hali hii zoezi la kuwanusuru ndugu zetu wasomali na baa hili la njaa limeingia dosari,hivyo tuzidi kuomba miujiza ili Alshabab wasitishe mapigano na watoto,vijana na wazee wa Somalia wanusurike na njaa inayowakabili.
  

No comments: