Ile hali ya kuwepo kwa binadamu walio tofauti na wengine inaendelea kuongezeka,kwani huko Croatia kaskazini mtoto wa miaka 6 aitwae Ivan Stoiljikovic ambaye amekuwa na hali ya kunasa vitu vya chuma (usumaku) katika kiwiliwili chake.Mtoto huyo ambaye pia kimwili umbile lake halilingani na umri,hilo halimpi halimzuii kuvua chati na kuwaonyesha watu uwezo wake huo wa ajabu.
Babu aitwae Ivan Surlovic anasema,alinza kuonesha maajabu tokea akiwa mdogo kwani alianza kutembea akiwa na umri wa miezi nane,na kabla ya kufikisha miaka miwili alikuwa na uwezo wa kuendesha baiskeli,kitu ambacho kiliwashangaza.Babu yake anaendelea kusema, hali hiyo ya usumaku waligundua miezi michache iliyopita,wakati walipokuwa wakiangalia kipindi cha televisheni kilichokuwa kinamuonyesha kijana mwingine mwenye uwezo kama huo,nae Ivan ajijaribu kama utani, ghafla wakaona vitu vya chuma vinanasa pia kwake.
Familia yake inasema,hali hiyo huwa na nguvu zaidi nyakati za asubuhi akiwa ametulia,pia vyuma vizito hunanasa vizuri zaidi ya vile vyepesi.
Nzito lakini hapa ndo imenasa. |
"Jamani ona mikono yangu ipo nyuma,sijaichika" |
No comments:
Post a Comment