Azerbaijan ni moja ya nchi zinaongoza kwa uzalishaji na uuzaji mafuta dunia. Katika mji wake mkuu Baku, kumetokea hospitali inayojulikana kwa jina la Naftalan ambayo kwa miaka mingi sasa imekuwa ikitumia mafuta ghafi kama tiba ya magonjwa mbalimbali ya ngozi na mengine ya viungo na mifupa kama arthititis na rheumatism . Katika tiba hiyo mgonjwa hutakiwa kujiloweka katika sinki lenye gallon 35 za mafuta hayo na kukaa ndani yake kwa muda usiozidi dakika kumi.Wagonjwa wengi wamesema hujisikia vizur wakati wapo ndani ya mafuta hayo hivyo kutamani kukaa zaidi ya dakika hizo zinazopendekezwa na daktari. Meneja mkuu katika hospitali hiyo, Dr Alif Zulfugar amesema kuwa mgonjwa hatakiwi kuzidisha dakika pia haruhusiwi kutumia tiba hiyo zaidi ya mara moja kwa siku kwani inaweza kumletea madhara ambayo hakuyataja.Ameongeza kwa kusema tiba hiyo inatolewa kwa muda wa siku 10 tu.
|
Baadhi ya wagonjwa wakioga dawa hiyo |
|
Jamaa akifutwa mafuta hayo baada ya kujiloweka |
No comments:
Post a Comment