Homa matokeo kidato cha 6...sintofahamu yazidi kwa watoto wa wakulima


Zikiwa zimebakia siku chache kwa matokeo ya kidato cha sita 2012 kutoka, homa”   juu ya hatima ya vijana waliofanya mtihani huo imezidi kuongezeka. Joto hili limezidi kuongezea sio tu kwa kuhofia ufaulu wa mtihani yao bali kilichoongeza sintofahamu ya  hatma yao kwenda vyuoni, wengi wahofia kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu kwani hali ya kupata ufadhili kutoka bodi ya mikopo (HESLB) umeanza kuonekana  kuwa mgumu (tete).

Kukata tamaa huku kumechangiwa zaidi na taarifa zilizotolewa na TCU kupitia kitabu cha mwongozo wa udahili 2012/2013-Admission guide book 2012/2013. Katika kitabu hicho ambacho licha ya kutoa vigezo vinavyohitajika ili mwanafunzi achaguliwe kwenda kusoma katika chuo husika pia wametoa mchanganuo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013. Katika mchanganuo huo  unaonyesha vipengele viwili ambavyo ni Possible Loan amount na Loan Priority. Katika kipengele cha loan priority kinaonyesha kozi (taaluma) ambazo zimepewa kipaumbele cha kupewa mkopo, hivyo kupelekea kuwepo kwa makundi mawili ambayo ni Priority na Non Priority. Kwa ufupi non priority ni wale ambao hawana uwezekano wa kupata mkopo. Hivyo possible loan amount kinawahusu wale ambao ni priority (watakopata mkopo)

Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba asilimia 96 ya kozi zote zinazotolewa na vyuo mbalimbali ni non priority isipokuwa kwa wataochagua Education, Engineering na Medicine,Kilimo na kozi nyingine baadhi za sayansi. Hiki ni kizungumkuti kwa wale waliokuwa na matumaini ya kusoma Biashara, Uchumi, Political Science, Sheria, Uandishi wa Habari, na kozi nyingine zilizobaki kwani upatikanaji wa mikopo kwao ni ndoto. Sijui ndugu zangu watoto wa wakulima waliosoma EGM, HGE, HKL, HGL, HGK KLF nk watakimbilia wapi? Kimbilio liliobaki ni education pekee, tena watakaomudu kusoma hii  ni wale waliotoka kwenye familia zenye auheni kidogo (middle class) kwani bodi wanatoa ufadhili wa 50% kwa watakaosoma education;  lakini kwa mtoto wa mkulima choka mbaya kupata elimu ya chuo asahau.

Wazee wa IFM  mpo??chuoni kwenu hakuna kozi hata moja inayokula mkopo??
Uwezo wa kumudu gharama za ada, (tuition fee), chakula na malazi (meals & accommodation), na fedha nyingine za kujikimu zitapatikana wapi? Gharama hizi mzigo usiobebeka na wazazi wengi hawawezi kumudu gharama hizi. Hiki ni kilio, tena kisicho na mfiwa maalumu..wafiwa ni watoto wa masikini ambao ni tuko wengi hapa Tanzania. Kwa hali hii watakaosoma vyuo ni watoto wa matajiri tu! watoto wa wakulima twende wapi?  kwenye mabenki tukachukue mikopo ya kujisomesha? Inasikitisha kuangalia kitabu hicho cha TCU. 
Hii ni chinja chinja mpaka wazee wa Mzumbe panga hili limewapitia
Nashindwa kuelewa nini maana ya mkopo?hivi fedha hizi si hurudishwa pindi mwombaji anapomaliza masomo? Au ndo serikali haina fedha kama tunavyosikia? Huku ni kutowatendea haki watoto wa masikini walio na kiu ya kupata elimu ya juu. Tena ni uonevo mkubwa..njooni vyuoni mtazame maisha ya wanafunzi wa mwaka jana waliokosa mkopo..maarufu kama NO LOAN…nadhani kupitia hili umuhimu wa kuwapatia wanafunzi mikopo unaweza kuonekana. 
Sio kwenu tu IFM ndo hakuna mkopo?vyuo kibao kama CBE,Ustawi, Tumaini,KIU,bodi hawatoi mkopo pia



Matokeo hayo ya kidato cha sita yanatarajiwa kutoka mwisho mwa mwezi huu kama ilivyo ada. 
Wazee wa SUA

HILL mpo??



Itazame hii halafu unipe maelezo!!

Hebu iangalie na wewe hii picha kwa sababu nimeshindwa kuitolea maelezo..(caption)!!Pia sifahamu kilichokuwa kinawaliza hawa  watoto..jaribu ku-share na sisi kilichopo kichwani mwako.

Bi Joyce Banda rais mpya Malawi.

Aliyekua makamu wa rais wa nchini Malawi,Bi Joyce Banda ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.Hii imekuja kufuatia kifo cha raisi Bingu wa Mutharika.  Banda anakuwa rais wa kwanza wa kike kusini mwa Jangwa la Sahara, na amepishwa mbele ya bunge katika mji mkuu wa Lilongwe Malawi.
Bi Joyce Banda rais wa kwanza mwanamke kusini mwa jangwa la sahara

Bi Banda, ambaye alikuwa makamu wa rais tangu mwaka 2009, alishangiliwa na kupigiwa kofi kabla na baada ya shughuli hiyo. Bw Mutharika, 78, alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Alhamis, ingawa kifo chake hakikuthibitishwa hadi Jumamosi. Kuchelewa kutangazwa kifo chake kulisababisha wasiwasi kuhusu nani anaongoza nchi hiyo. Kulikuwa na tetesi kuwa watu wa karibu wa rais Mutharika walikuwa wakitaka kubadili katiba ya nchi ili kuzuia Bi Banda kuchukua madaraka, na badala yake kumpa ndugu yake, Peter Mutharika ambaye ni waziri wa mambo ya nje. Bi Banda alifarakana na rais Mutharika mwaka 2010 na kuwa mkosoaji mkubwa wa rais. Alifukuzwa kutoka chama cha DPP na kuunda chama chake cha Peoples Party

Kauli ya Hussein Bashe kuhusu ushindi wa Arumeru


Kwanza nitumie nafasi hii binafsi kuwapongeza CHADEMA kwa ushindi wa Arumeru Mashariki, Kiwira, Kirumba, Liziboni na Pia CUF kwa ushindi wa Kata ya Tanga

Nimeamua kufanya hivi kwa misingi ya kidemokrasia ni wapongeze mmepewa heshima hiyo watumikieni.

Nawapongeza pia kwakua uchaguzi huu kama viongozi wa CHAMA changu watatumia Busara basi hili ni funzo kubwa, na nina washukuru CDM (chadema) matokeo haya kutupa ishara kuwa Kaskazini inaanza kupotea mikononi mwetu, Kusini Nyanda za Juu inaanza kupotea, Kanda ya Ziwa inaanza kupotea hii ni Alarm kwa CHAMA change, umewadia wakati kwa ujumbe huu viongozi wakuu warudi katika Round Table kujadili upya na kutazama kama makundi yetu yatakisaidia CHAMA


Kwa matokeo haya Kanda ya ziwa alikuwepo Samwel Sitta ,kwa maana ya Kirumba, Mbeya alikuwepo Mama Anne Kilango, kwa Maana ya Kiwira, Arumeru alikuwepo Mzee MKAPA, Mzee Mkama, Mzee Lowasa, Ndg yangu Nape, Liziboni Dk Nchimbi na maaneo haya yote, Tumeshindwa umewadia wakati wa KUJITAFAKARI na kujiangalia kwa kina na si kuja na majibu kama yale tuliokuja nayo Baada ya Uchaguzi Mkuu 2010, Tunatakiwa kuja na MAJAWABU.

Nadhani demokrasia imeheshimika na CCM tumekua tukisahau wajibu wetu wa kujadili matatizo ya watu toka mwaka 2007 Mpaka sasa 2012 , wananchi walitupa 1st Workup call 2010 hatukuamka and this is a 2nd Workup Call hatuna Budi kuwashukuru wananchi bcs Wametupa 2nd chance ya kuamka Tujitafakari UPYA

Nimelizie kuwwapongeza CUF na CDM kwa Ushindi wao niwatakie kila la kheri Asanteni kwa kutuamsha mara ya pili.

kwa hisani wavuti

Field hazishikiki!!Ajira hazionekani!!huu msiba unakuhusu..

   Kweli daima itatuweka huru, inashangaza kuona  malumbano juu ya kauli ya iliyotolewa hivi karibuni na waziri mkuu mstaafu Mh, Edward Lowassa kuwa tatizo la ajira nchini ni bomu linalosubiri kulibuka!!Kiukweli nashindwa kuelewa yanatokea wapi kwani tatizo hili liko wazi kabisa..nashawashangaa pia watu wanaojitahidi kupindisha ukweli katika hili ilhali ukweli unajulikana..cha kusikitisha kada wa Umoja wa Vijana CCM anathubutu kumkejeli Mh Lowassa eti aonyeshe mikakati alioifanya kupunguza tatizo la ajira wakati alipokua waziri mkuu!!Hii ni kejeli na mzahaa usiotakiwa wakati mambo yanayougusa umma yakijadiliwa. Au ni kwa sababu tu Lowassa ndo amezungumza basi imekua nongwa?!!Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..Kiukweli ajira ni issue (tatizo), tena sio bomu linalosubiri kulipuka bali tayari limeshalipuka na  kilichobaki ni kuona madhara yake.

  Katika kudhihirisha kuwa tatizo la ajira nchini ni kubwa kwanza tuanze kuangalia namna ya upatikanaji wa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) kama inavojulikana kwa wengi. Kwa utafiti mdogo uliofanywa katika vyuo vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria, College Business Education imebanika kuwa kati ya wanafunzi kumi,saba kati yao wamekiri kabisa kukosa nafasi za field sio tu kwenye taasisi binafsi hata zile za serikali. Ugumu huu umekua kikwazo sana kwa wanafunzi wanaosoma taaluma nyingine tofauti na ualimu kwani upatikanaji wao huwa ni rahisi kwani vyuo vingi mawasiliano na shule husika ambazo wanafunzi wanataenda kwa ajili ya mafunzo.

   Sababu husika ya ukosekanaji wa nafasi hizi imebainika kuwa ni urasimu uliopo kwenye taasisi hizo. Mwanafunzi unaweza kupeleka barua kwenye ofisi na barua hiyo isipokelewe kabisa na unapewa majibu kwamba hapa hatunaga mambo hayo..yaani hawapokei wanafunzi wa field..kwingine barua inapokelewa lakini majibu hayatolewi unatafutilia kutwa kucha mwishowe watakujibu we don’t have the chance to accommodate you!! Kwingine utambiwa samahani barua yako haionekani jaribu kuileta tena..Kiukweli hali hii inakatisha tama kwani mwanafunzi huzunguka hadi muda wa miezi miwili bila mafanikio. Pia kuna baadhi ya ofisi ambazo zinajulikana kabisa kuwa chuo fulani hakipokelewi kwa nafasi za field..utajibiwa hapa hatupokei Open na Ustawi nafasi zipo kwa vyuo vingine…Tukapate wapi hayo mafunzo kwa vitendo wakati nafasi zenye hazipatikani? Chakujiuliza kama field ni zengwe kiasi hiki je hizo ajira inakuaje??ni wazi kwamba hata ajira ndo hazionekani kabisa.

   Kudhihirisha kuwa hili tatizo ni kuna baadhi ya watu wamegeuza deal na kufungua ofisi ambazo huwaunganisha wanafunzi na ofisi ambazo watahitaji kwenda kufanya field. Ilikumwezesha mwanafunzi kuingizwa katika mchakato wa kutafutiwa sehemu ya field huhitajika kulipia gharama ya shilingi elfu ishirini. Kwa upande mwingine kujuana, undugu na rushwa hasa za mapenzi kwa akina dada imebainika kuwa ni siri ya kupata nafasi kwenye baadhi ya ofisi. Pia imegundulika kuwa sehemu nyingine huofia kuwalipa wanafunzi!!!

  Halikadhalika wanafunzi wametakiwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani utovu wa nidhamu imekua ni sababu nyingine pia ya wanafunzi kukosa nafasi za field. Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa moja ya vitu vinavyoongeza stress na ugumu katika maisha ya uanafunzi ni suala la field, hivyo wadau husika wa taasisi mbalimbali wanaombwa kufungua milango ya field kwani kufuatia ugumu huu imepelekea baadhi ya wanafunzi kutofanya kabisa field!!

Tafakari...unipe maoni yako!!

Katika pitapita yangu kwenye mitandao nimekumbana na habari moja yenye kichwa cha habari Wanafunzi chuo Kikuu Cha Dar es Salaam "Wanasikitisha” . Kama kichwa cha habari kinavyovutia basi nami nikaamua kuipitia…..Kiukweli nimesoma mpaka mwisho…habari hiyo ime-click kichwa changu,cha ajabu nimeshikwa na kigugumizi nikakosa la kusema!!!
Picha iliyoambatanishwa kwenye habari hiyo
   Nakuletea habari hiyo wewe kama mdau wa elimu ya juu hapa Tanzania hususani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unipe maoni yako…...

Habari kamili;

  • Kabla hamjaanza kunirushia "mawe" inabidi nianze kwa kusema kwamba hii siyo kauli yangu. Ni kauli ya mwanafunzi wa Kimarekani aliyekuwa anafanya utafiti kwa ajili ya tasnifu yake ya uzamili kule Zanzibar na Dar es salaam. Mwanafunzi huyu pia alikuwa anahudhuria mihadhara michache ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
  • Alipotoa kauli hiyo hapo juu nilishtuka sana. Nilifikiria ni yale yale ya mababu zake waliokuja Afrika na kuanza kutuhukumu kwamba Waafrika tulikuwa na tamaduni za kipumbavu; na kwamba ustaarabu ulikuwa umetupiga chenga. Ilibidi nimsikilize kwa makini wakati alipojaribu kufafanua kauli yake hii. Kimsingi hoja yake ilikuwa imeegemezwa katika mambo yafuatayo:
(1) Lugha ya Kiingereza
  • Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam hawawezi kuendesha mazungumzo ya maana kuhusu jambo lolote katika lugha ya Kiingereza. Pamoja na shauku kubwa ya kutaka kumwonyesha wema na kumwingiza katika mazungumzo ya aina mbalimbali, Kiingereza cha wanafunzi wengi wa Mlimani kilikuwa kibaya kiasi kwamba wengi wao waliishia kumkodolea macho tu. Alisema kwamba alijisikia vibaya sana na alijaribu kutumia Kiswahili chake kibovu huku akichanganya na Kiingereza. Aliniomba nitoe maoni yangu kuhusu sababu zinazosababisha umuduji hafifu wa Kiingereza kwa wanafunzi wa chuo kikuu.
  • Baada ya kumpa maoni yangu ambayo yalijumuisha sera yetu tatanishi ya lugha ya kufundishia na changamoto zingine katika mfumo wetu wa elimu, nilijaribu kumchokoza kwa kumuuliza ni kwa nini alikuwa anategemea wanafunzi hawa kufahamu Kiingereza. Mbona yeye hakujiandaa vyema na kujifunza Kiswahili vizuri kabla hajaja kufanya utafiti wake? Aliniambia kwamba Kiswahili alichojifunza kilikuwa kinatosha kuuliza maswali yake hojaji (questionnaires) na kurekodi majibu aliyohitaji. Aliendelea kuniambia kwamba hakuendelea kujifunza Kiswahili zaidi baada ya kugundua kwamba Kiingereza kilikuwa ni lugha ya kufundishia na alitegemea kwamba wanafunzi hawa wangekuwa wanaifahamu vizuri lugha hiyo ya kufundishia.

(2) Maprofesa
  • Kimsingi alisema kwamba hakujifunza chochote cha maana na anajihisi kama vile pesa za ada alizolipa zilikuwa zimeenda bure tu. Maprofesa ni haba sana na waliopo inaonekana wameelemewa na wingi wa wanafunzi. Kwa mfano, profesa wa darasa lake hakufika kwa karibu wiki zote nne za mwanzo wa muhula na hata alipofika alisema kwamba alikuwa amepangiwa kipindi kingine katika wakati ule ule aliopaswa kufundisha darasa la hawa Wazungu kutoka Marekani. Inaonekana Profesa alichagua kufundisha darasa la Watanzania kwani Mmarekani huyu alidai kwamba darasa lao halikukutana zaidi ya mara nne kwa muhula mzima.
  • Mara nyingine Profesa alipiga simu na kuwaambia wanafunzi waliokuwa wakimsubiri darasani kwamba alikuwa amekwama katika foleni ya magari, gari lake lilikuwa limeharibika na visingizio vingine. 
  • Tuliongea mengi kuhusu suala hili na nilijaribu kumwambia kwamba hali ya hewa ya kimasomo Mlimani inaweza kuonekana kuwa legevu hasa katika wiki mbili za mwanzo lakini ikija kuchangamka huko mbele ni moto mtindo mmoja. Alicheka tu na kusema kuwa si kweli. Yeye alikuwa haamini kama wanafunzi wale walikuwa wanasoma wanachopaswa kusoma; na alikuwa haamini kama kweli wanafunzi wetu wanaweza kupambana katika soko la ajira la Kimataifa!

(3) Matatizo ya Kimiundo mbinu 
  • Mfano udogo wa vyumba vya madarasa, wanafunzi wengi kupita kiasi, ukosefu wa maji na umeme mabwenini, ukosefu wa vitabu vya kisasa na matatizo mengine. Aliniambia kuwa matatizo haya ni "self explanatory" na alikuwa anayategemea ingawa katika baadhi ya mabweni hali ilikuwa mbaya sana.
  • Aliendelea kudai kwamba safari yake hii ya Tanzania ilikuwa imebadili kabisa mtazamo wake kuhusu mkakati mzima wa  maendeleo ya Afrika. Alisema kwamba kutokana na aliyoyaona ikiwemo tabia ya kutojali, uvivu na kutorekebisha hata mambo madogo madogo tu, anafikiri kwamba kipingamizi kikubwa cha maendeleo ya Afrika ni Waafrika wenyewe. Alisema kwamba safari yake hii imembadili mawazo kiasi kwamba ameamua kuitelekeza mada yake ya mwanzo na ameamua kuandika tasnifu ya Uzamili na Uzamivu juu ya mikakati ya maendeleo katika bara la Afrika huku akitumia Tanzania kama eneo rejea. Na kuanzia sasa atapinga sana mawazo yaliyotawala ya kujaribu kuiendeleza Afrika kwa kuipa misaada na mikopo ya kifedha. Tumepanga kukutana tena na kuzungumza juu ya changamoto za Kisiasa na kijamii alizoziona.
Swali

Ati, kuna ukweli wowote katika hoja za mwanafunzi huyu mpekuzi? Ni kweli Waafrika tu wavivu na tusiojali; au watu wa nje hawatuelewi sisi na mfumo wetu wa maisha? 

Naomba maoni yako mdau
Habari imetoka globalpublishers

Wanaume nchini Kenya waandaa mgomo wa kutokula majumbani mwao!!

Kufuatia malamimiko ya muda mrefu ya kupokea kipigo kutoka kwa wake zao, wanaume nchini Kenya wamepanga kufanya mgomo wa kutokula majumbani mwao kwa muda wa wiki moja. 
kiAtoa rai hiyo Kiongozi wa chama cha kutetea wanaume Bw Nderitu Njoka amesema,badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni.
Aidha Bw  Nderitu amesisitiza kuwa kuanzia leo jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akina baba kula mahotelini badala ya majumbani mwao.Ameongeza kuwa mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.
Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wauaume alikuwa akizungumza katika hospitali kuu ya mjini Nakuru huko Rift valley ambako alikuwa amekwenda kumjulia hali baba mmoja ambaye amelezwa  kutokana na kipigo alichopewa na mkewe.
Bw Njoka akimpa pole baba aliepigwa na mkewe
Baba huyo akizungumza kwa uchungu hospitalini alisema mkewe alimuita nyumbani ili akachukuwe pesa kabla ya kumfungia chumbani na kumtandika.
Kwa mujibu wa bwana Nderitu Njoka, mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopigwa na bibi zao. Katika mkoa huo wa kati wanaume karibu nusu milioni wameripoti kupigwa na wake zao. Chama hicho cha wanaume kimedai kuwa kuna wanaume ambao wanalazimishwa kufua nguo za wake zao. Wengine pia wamelalamika kunyimwa tendo la ndoa na mabibi zao.
Jijini Nairobi wanaume ambao huona kivumbi kutoka kwa wake zao ni laki tatu.
Lakini baadhi ya akina mama kutoka mkoa huo wanasema akina baba ndio wa kulaumiwa kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ya kifamilia.
Wanasema waume wengi wamekuwa "wanaume suruali" tu.
Hata hivyo wengi wanasubiri kuona kama kweli mgomo huo utafaulu, na ni wanaume wangapi walio na pesa za kwenda kula hotelini badala ya kula majumbani mwao.

source bbc swahili

Tamko la BAVICHA kuhusu wanafunzi waliofukuzwa vyuoni.

       Kwa miaka ya hivi karibuni Vyuo mbalimbali vimekua na tabia yakuwafukuza ama kuwasimamisha masomo wanafunzi wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini mwetu kutokana na mashinikizombalimbali kutoka kwa viongozi wa kiserikali kwa kisingizio kuwa wanafunzi hawa wanafanya siasa vyuoni.Itakumbukuwa kuwa migomo na maandamano ya wanafunzi kwa vyuo vikuuhapa nchini haijaanza pale mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa kuanzamwaka 1992 ,bali migomo na maandamano haya yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa vyuo hivyo.Mathalani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa na historia ya migomo na maandamano ya mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake , na hivyo dhanaya kuwa wanafunzi wanagoma kutokana na misukumo ya kisiasa sio sahihihata kidogo bali ni mbinu ya watawala kujaribu kuficha madhaifu yao .Wanafunzi hawa wamekuwa wakigoma kutokana na serikali ya CCM kuendeshamambo yake kibabe na kwa dharahu ya hali ya juu ambapo imefanya elimukuwa Privilage na si haki kwa watanzania.

Kwa mantiki hiyo basi, kutokutendewa haki kwa wanafunzi hawa naserikali yao, kukosekana kwa miundombinu bora ya kusoma na kujifunzia,wanafunzi hawa kunyanyaswa na watawala wa vyuo hivyo, kukosekana kwamikopo kwa wakati muafaka, serikali kuingilia uendeshaji wa vyuo ,serikali kuvunja serikali za wanafunzi bila kutoa sababu za kimsingi na sababu nyingine mbalimbali ndio chanzo cha vurugu na migomo vyuoni.

Hivyo basi , kutokana na sababu tajwa hapo juu Baraza la Vijana na CHADEMA (BAVICHA) tunatamka wazi kuwa kitendo cha Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam, Dodoma na Muhimbili kuwafukuza wanafunzi kwa ujumla wakez aidi ya 100 ni kitendo cha uonevu kwa wanafunzi hawa na kamwe hakivumiliki hata kidogo na haswa ikizingatiwa kuwa ni watoto wa watu masikini na ambao kimsingi wanajilipia ada wenyewe kwani wanakopa na baada ya muda watapaswa kulipa fedha hizo.
Kwa nini tunapinga uamuzi huu wa kuwafukuza wanafunzi vyuoni;
 
1. Ni kinyume na Tamko la Ulimwengu la mwaka 1990 la uhuru wa kitaaluma (Academic Freedom) ambalo tulisaini mnamo mwezi April tarehe29 hapa Dar Es Salaam , linasema wazi kuwa ni lazima Vyuo vijiendeshe kwa uhuru kamili bila kuingiliwa na serikali .
2. Kufukuzwa kwa wanafunzi hawa ni utekelezaji wa Maazimio ya vikaovya CCM vilivyofanyika na haswa vile vya Halimashauri Kuu ambavyo vimetoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali juu ya kuwachukulia hatua wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali waziwazi ,na hata wahadhiri ambao wamekuwa wakitumia taaluma zao kwa uwazi nakusema juu ya mapungufu ya serikali wachukuliwe hatua ya ama kufukuzwa kazi  au ajira zao kusitishwa. Hivyo hii ni muendelezo wautekelezaji wa maamuzi hayo. 


Nothing to stop you,just do it!!


 Nimesimama tayari kwa kuanza kufanya, lakini sijui nianzie wapi? Sio kama sijui  ninachotaka kukifanya, HAPANA!!nakifahamu fika ,tena akili  imelipangilia jambo hilo vizuri, tatizo macho yanaona lakini  hayaoni mwanzo wake!! Mikono na miguu ina nguvu lakini vimepatwa na kigugumzi haviwezi kufanya lolote!!  Chakusikitisha  domo langu gundi linashindwa kusema, ili nisaidiwe kuoneshwa mwanzo eti kisa nafsi inaogopa kuchekwa!  

   Hofu imezidi kuingia nafsini,  tena nazidi kuogopeshwa kwa lugha ya kizungu eti “time will tell” kwa tasfiri rahisi wanamaana eti nisubiri mpaka muda utakapozungumza! tangu lini muda ukawa na mdomo ?! tena sijui unazungumza lugha gani? Ghalfa nawakumbuka wahenga, wanananiambia “ngoja ngoja ya huumiza matumbo!” nami naingiwa na hofu ya kuumwa tumbo. Akili inazidi kufunguka na kuuona kuwa wakati ni ukuta, hivyo hakuna wakati mwingine wa kuyafanya haya. Muda ndo huu, akilini inakemea hofu, nguvu ya uthubutu inajaa nafsini, mara napokea muujiza, macho yanaona mwanzo mpya, mikono na miguu viko tayari kufanya kazi! Gundi lililojaa mdomoni linayeyuka ghalfa napata kusema, wengine wanadharau na kuona kile ninachotaka kufanya hakina maana, Sivunjiki moyo! wapo wanaonipa moyo nakuona uzuri wa kile ninachotaka  kufanya. Nainza safari ya kufanya, nilikuwa sioni mwanzo lakini sasa nauona. Safari inaendelea tena kwa mwendo wa LORUUU KEIKEI….sijali vikwazo vya njiani mpaka nitakapofika kwani siku zote “the end justify the means” kwani mwisho ndio utakaonipa majibu ya hiki ninachokifanya.

  Wengi tunateswa na ugonjwa huu,ni gonjwa la HOFU inasemekana wengi tunaugua ugojwa huu! mambo yetu mengi hayaendi kisa hofu, wengine stress (msongo wa mawazo) zinazidi kisa hofu. Dawa imegundulika kuwa ni kujipa moyo, uthubutu na kujiamini. Kataa hofu na if you want to do, DO IT NOW hakuna wakati mwingine.


Kila ufikiriapo ndipo mafanikio yako huongezeka!!!


Tukumbuke ndugu zangu,mawazo ndiyo mwanzo wa mafanikio yako. Unapokuwa na ndoto mafanikio kwanza yakupasa kuwa na wazo ambalo baadae utalifanyia kazi, ili utengeneze bahati yako. Kwa kufuata maelekezo hayo utakuza upeo wa fikra zako.

Wengi wanaweza wasikutendee haki, kama wengi wafanyavyo, wanaweza kukupotosha katika uhuru ulionao, lakini hawawezi kukuchukulia mawazo unayoyawaza. Kutokana na fikra zako utakuwa unashinda siku zote. 

Unataka kuwa na furaha? Unataka kuwa na amani? Unataka kuwa na cheo, nguvu au utajiri? Fikiri kuwa navyo, utafanikiwa. Fikra unazowaza ni muhimu kuliko ujuzi ulionao. 
Ujuzi una mipaka, mawazo yanatawala muda wote, yanaleta maendeleo. Kila mtu binafsi anakuwa na ndoto za mafanikio bila kujitambua. Kwa mfano, wazazi wanapopanga ni jinsi gani watawaendeleza watoto wao, wajasiriamali wanapopanga ni jinsi gani wataendeleza biashara zao hiyo yote ni mifano ya kuwa na ndoto njema ya mafanikio. Watu wachache wamejifunza kutumia mawazo yao kwa faida lakini wengi wetu mawazo tuliyonayo yanapata kutu kutokana na kutoyafanyia kazi. Hakuna sababu ya kuona aibu katika dunia ya ubunifu.

Kuwa na mawazo ya kufanya jambo fulani ni kitu kizuri katika dunia hii tunayoishi. Kila mmoja wetu ana kiwanda chake cha kuwa na mawazo. Lakini ni wapi mawazo hayo yanapotoka? Ni wapi waandishi, wana sayansi na wabunifu wanapopata mawazo makubwa? Kwa nini baadhi ya watu wengine wanakuwa wabunifu zaidi ya wengine? Ni kutokana na kutumia vizuri mawazo yao.

 Kila mmoja wetu, kwa wakati mmoja au mwingine, lazima kujifunza chanzo halisi cha mawazo. Utajiri, unaweza kuupata, inategemeana na ulivyoyaweka mawazo yako. Wazo dogo rahisi linaweza likabadilisha kabisa maisha yako uliyonayo.  Pia huwezi ukajua ukubwa wa mafanikio yako mpaka utakapojifunza jinsi ya kuchanganya juhudi zako na mawazo yako.  Kwa vyovyote unapotaka mafanikio unajitathmini wewe mwenyewe. Mwili uliopumzika una nguvu, vile vile akili. Kama unataka kuwa mbunifu na mpokeaji wa mawazo mapya, inakubidi kupata muda kwa mawazo hayo na kuyafanyia kazi.
Jizoeze kila siku kuwa na muda wa mapumziko, chagua chumba kizuri kilichotulia au kiti kizuri ambacho kitakusaidia kutuliza akili kwa urahisi. Unavyoendelea kujifunza kupumzika, utapata mawazo ambayo yatakufikisha katika malengo na matarajio yako.

Mtunzi anafikiri juu ya uimbaji, mchoraji anafikiri juu ya rangi, mwandishi anafikiri juu ya habari na maneno. Kama utachukua wazo moja na kulitendea kazi litakupa matokeo mazuri. Yafanyie kazi mawazo yanayokujia. Kuwa na utayari katika kunasa mawazo yako. Mawazo mengi mazuri yanapotea kwa sababu hayawekwi katika maandishi.

Tathimini mawazo yako. Mara tu unapomaliza kuyachuja mawazo yako, unachagua yale unayotaka kuyafanyia kazi. Utagundua kuwa nayo yanahitaji kuongezewa ubora wake. Jifunze ndugu yangu kutokufunga milango yako ya kuwa mbunifu.


Makala hii imetoka kwa Seif Kabele

UDPRSA 5th anniversary marked a new beginning!!

Celebration of the 5th anniversary of University of Dar es Salaam Public Relations Student Association (UDPRSA) has marked an opening way in which all UDPRSA members and other PR professional s in the industry to communicate and interact easily on matter concerning their career, this is due to the launching of their blog and face book page.

   While speaking to members the guest of honor and the main speaker his excellence Professor Eno Akipabio encourages leaders and members to be committed and insists leaders to come up with new ideas that will strengthen their association. He further said through such association will enable them to exchange their ideas, creating networks professionals and utilize the opportunities that face them as students. Prof Akipabio went on saying the opening of blog and facebook page is great achievement especially at this era of development of social and new media.
The display which shows UDPRSA blog
However, on his remarks Mr Amin Antony Mgeni who was among the founders of UDPRSA said he is happy to see the association still exists and he advise leaders to take quick solution to whatever challenge encounter the association. Mr Mgeni who is currently an editor at Mlimani tv, encourages members to use the blog in writing articles and feature stories hence would enable them to become good PR’s. 
On the left is Mr Kisoma Mussa and Mr Amini Mgheni one of the founder of UDPRSA
“This 5th anniversary is a challenge to me and my cabinet, we ensure that UDPRSA will still move on, but without your cooperation (members), UDPRSA won’t succeed” said the new President of UDPRSA, Mr Kisoma Mussa. He added that up to this time they succeed to create a network with association like University of Dar es Salaam Markerting Association (DUMA), Saut Student Public Relations Association (SSPRA) and currently they are in discussion with Public Relations Association of Tanzania to see on how they can work together.

From the left is UDPRSA vice president Mr Raymond,Bonnie-UDPRSA deputy GSProf  Akipabio and Kijanga
The 5th anniversary celebration was held on 10th November at School Journalism and Mass Communication and was attended by the Director of Publicity at DUMA, Mr Enock Ngulwa, media people and other alumni of SJMC.
UDPRSA members during 5th anniversary event.

HATUWEZI KUENDELEA KWA NCHI ILIYOJAA WANYOA VIDUKU!!

  Nafurahishwa sana kwa kuona muamko mkubwa wa Watanzania wengi  kutaka kuwa na maendeleo katika nchi yetu, hamasa hii inatokana  na kufunguka kifikra na kiakili miongoni mwa watu hivyo kupelekea kujitambua na kujua haki zao na kipi wa wanachokitaka  kiwepo katika jamii yetu. Lakini kwa masikitiko makubwa napenda kuwa vunja moyo kwa kuwaambia kuwa HATUWEZI kupata maendeleo kwa taifa lililojaa wanyoa viduku na wavaa supra!!” .   Najua unajiuliza kwani kuvaa supra na konyoa kiduku  kuna mahusiano gani na suala la maendeleo?? Sina  maana ya wazi kiiivo ,naamanisha kuwa suala la maendeleo hushangiwa kwa kiasi  kikubwa na kupevuka kwa fikra kwani hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa” Umasikini wa fikra ni umasikini mkali kuliko yote” lakini wengi wetu hasa vijana bado hatujataka  kuzipevua akili zetu bali tumezidi kuzidumaza fikra zetu kwa kufikiria kunyoa viduku,kuvaa  kata K, huku tuikimba Muhogo andazi, Muhogo andazi, na kwa sauti kubwa tunaimba ni sababu ya Ulofa na nyimbo nyingine za mahadhi hayo. Zaidi ya hapo tunafikiria ni lini tutaenda kupiga picha za editing kule my fair au photo point! Kubali kataa hayo ndio mawazo ya sisi vijana wa leo. Mfano mzuri ni wengi wa wanamuziki wetu vijana hawatoi nyimbo zenye hamasa kwetu.

KATIKA HILI WATANZANIA TUMEMSAHAU GADDAFI!!

  Inaelekea waTanzania wengi wamesahau historia kati ya Libya na Tanzania. Marehemu Gaddafi alikuwa rafiki yake mpenzi nduli mshenzi Dikteta Idi Amin Dada wa Uganda!  Gaddafi alitaka Amin amwoe binti yake! Gaddafi alituma wanajeshi kutoka Libya kuwasaidia Uganda katika vita vya Kagera mwaka 1978-79.  Sisi wazee tunaikumbuka hio vita na miezi kumi na nane (miaka 18) ya shida iliyofuata!  Maoni chini yameandikwa na mwanachama la kundi - Wanabidii

Kanali Gaddafi alipotembelea Uganda mwaka 1978

...Wanabidii!


  
Binafsi nachukia sana kuandika bila ya ushahidi! Na zaidi sipendi kuandika "propaganda" na taarifa za uzushi; isipokuwa napenda kuandika taarifa zilizotafitiwa kwa kuandikwa na mtafiti mwenyewe (na au mwandishi aliyeandika matokeo ya utafiti au kufanya upembuzi wa utafiti husika). Takriban wiki moja sasa (tangu Alkhamis ya tarehe 20 Oktoba, 2011) uwanja wa "Wanabidii" na majukwaa mengine ya kijamii yamekuwa yakijadili "Kuuawa kwa Kanali Muammar Gaddafi" kulikofanywa na wale wanaoitwa waasi (wa NTC) wakisaidiwa na NATO wakiongozwa na Uingereza, Marekani, Ufaranza na washirika pamoja na Waarabu (Saudia na Qatar). Gaddafi ameuawa; kwa jinsi gani, kila mmoja amesoma, ameona (kwenye picha za mndato) na au kwenye picha za video!

  
Ninachotaka kuandika na pengine kuanzisha "mjadala" wa kiakili ni juu ya "GADDAFI KUMSAIDIA IDI AMIN DADA KWENYE VITA VYA KAGERA [UGANDA DHIDI YA TANZANIA MWAKA 1978 HADI 1979]". Napenda niweke wazi kwamba, "historia haisomwi ili kufufua 'chuki' bali husomwa kujua yaliyopita, kuyasanifu yaliyopo na kupanga mipango kwa yajayo!". Hivi ndivyo tunavyosoma historia iwe yenye kuhuzunisha au kufurahisha! Tanzania ilipigana vita na Uganda, vita iliyoitwa VITA YA KAGERA (japokuwa ilipiganwa hata ndani ya Uganda na Idi Amini Dada kufurushwa na kuikimbia Uganda!).

Kwa ujumla, tangu pale kifo cha Muammar Gaddafi kilipotangazwa kwa mara ya kwanza na kituo cha runinga cha Al-Jazeera na kukaririwa na vituo vingine na mashirika ya habari ya kimataifa kama BBC, CNN, Reuters, Xinhua, AFP, AP na IRNA (Press Tv) kumekuwa na mkanganyiko wa "mawazo" kwa wananchi wa Tanzania juu ya "hali" ya Gaddafi kisiasa katika mtazamo wa kifalsafa...hususan wengi wa wachangiaji kwenye mijadala hiyo wanamuona Muammar Gaddafi kama "shujaa" na "mwanamapinduzi" na "kiongozi mtukuka" na "aliyejitolea kuunganisha Afrika" na hata wengine kufikia kiasi cha kuonyesha kwamba hajawahi kutokea kama Muammar Gaddafi na hata kumpa "daraja" ya kuwa "Baba wa Afrika" na mshumaa uliyozimika! Hata hivyo wengi wamesahau kwamba ni Muammar Gaddafi ndiye aliyemsaidia Idi Amin Dada kwenye Vita vya Kagera! Naomba sasa tuangalie nini alifanya Gaddafi wakati wa vita vile.

Vita vinahitaji rasilimali watu (askari na wataalamu wa kijeshi), fedha za kuendeshea vita na zana (za kivita na za mawasiliano ya kivita). Kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinazothibitishwa na taarifa rasmi za kihistoria Muammar Gadafi alimpa Idi Amin Dada usaidizi ufuatao:

HOTUBA YA MBUNGE WA MONDULI, EDWARD LOWASSA KWA WAANDISHI WA HABARI OKTOBA 19, 2011

Ifuatayo ni hotuba ya waziri mkuu mstaafu amabaye pia ni mbunge wa Monduli muheshimiwa Edward Lowassa aliyoitoa mapema leo nyumbani kwake Monduli Arusha, wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari…….

    NDUGU wana habari nimewaita katika mkutano huu leo kwa sababu moja kubwa, kutoa ufafanuzi kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakitokea huku yakinihusisha mimi binafsi kwa namna ambayo sasa yanatishia ustawi na mshikamano wa kimaadili, kihistoria na kikazi miongoni mwa viongozi na baina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

    Ndugu wana habari, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu habari zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazolihusisha jina langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baada ya kuwa zimesharipotiwa katika vyombo hivyo vya habari.

  Uamuzi wangu wa kukutana nanyi leo hauna makusudi ya kuzozana na vyombo vya habari wala kwenda kinyume na utamaduni wa kimaadili wa ndani ya chama changu unaotutaka viongozi kujadili masuala yanayokihusu chama chetu ndani ya vikao vyetu rasmi vya kimaamuzi bali kutoa ufafanuzina angalizo kwa pande zote hizo mbili ambazo zinaguswa na matukio yanayoendelea kutokea leo hii.

  Moja ya mambo ambayo yameligusa jina langu kwa namna hiyo ni lile linalonihusisha eti na kundi moja la wanasiasa ambao wamekuwa na mikakati ya kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Hakuna shaka ni madai ya kipuuzi, kizushi na yenye malengo machafu.

  Hawakuishia hapo sasa wamefikia hatua ya kuvitumia vyombo hivyo hivyo vya habari na kufikia hatua ya kudai kwamba nimeanza kuandaa orodha ya kile wanachokiita madhambi ya Rais Kikwete ambayo wanadai nimepanga kuyasoma wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CCM).

  Ninaamini kwa dhati kabisa kwamba, waandishi wa habari wanaofuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa masuala ya kisiasa nchini wanatambua kwamba, watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo kwa malengo ya kufikirika ya kujisafishia njia kisiasa.

  Ni jambo lisiloingia akilini kunihusisha na kile kinachoitwa mikakati ya kumhujumu rais