Nimesimama tayari kwa kuanza kufanya, lakini sijui nianzie wapi? Sio kama sijui ninachotaka kukifanya, HAPANA!!nakifahamu fika ,tena akili imelipangilia jambo hilo vizuri, tatizo macho yanaona lakini hayaoni mwanzo wake!! Mikono na miguu ina nguvu lakini vimepatwa na kigugumzi haviwezi kufanya lolote!! Chakusikitisha domo langu gundi linashindwa kusema, ili nisaidiwe kuoneshwa mwanzo eti kisa nafsi inaogopa kuchekwa!
Hofu imezidi kuingia nafsini, tena nazidi kuogopeshwa kwa lugha ya kizungu eti “time will tell” kwa tasfiri rahisi wanamaana eti nisubiri mpaka muda utakapozungumza! tangu lini muda ukawa na mdomo ?! tena sijui unazungumza lugha gani? Ghalfa nawakumbuka wahenga, wanananiambia “ngoja ngoja ya huumiza matumbo!” nami naingiwa na hofu ya kuumwa tumbo. Akili inazidi kufunguka na kuuona kuwa wakati ni ukuta, hivyo hakuna wakati mwingine wa kuyafanya haya. Muda ndo huu, akilini inakemea hofu, nguvu ya uthubutu inajaa nafsini, mara napokea muujiza, macho yanaona mwanzo mpya, mikono na miguu viko tayari kufanya kazi! Gundi lililojaa mdomoni linayeyuka ghalfa napata kusema, wengine wanadharau na kuona kile ninachotaka kufanya hakina maana, Sivunjiki moyo! wapo wanaonipa moyo nakuona uzuri wa kile ninachotaka kufanya. Nainza safari ya kufanya, nilikuwa sioni mwanzo lakini sasa nauona. Safari inaendelea tena kwa mwendo wa LORUUU KEIKEI….sijali vikwazo vya njiani mpaka nitakapofika kwani siku zote “the end justify the means” kwani mwisho ndio utakaonipa majibu ya hiki ninachokifanya.
Wengi tunateswa na ugonjwa huu,ni gonjwa la HOFU inasemekana wengi tunaugua ugojwa huu! mambo yetu mengi hayaendi kisa hofu, wengine stress (msongo wa mawazo) zinazidi kisa hofu. Dawa imegundulika kuwa ni kujipa moyo, uthubutu na kujiamini. Kataa hofu na if you want to do, DO IT NOW hakuna wakati mwingine.
No comments:
Post a Comment