Ndoto
ya wengi ni kupata kazi za kipato kizuri na ambazo zitawawezesha kuishi vizuri,
kumiliki gari, kujenga nyumba na mambo mengine lukuki.
Hata
hivyo, baadhi wamekumbana na tatizo la ajira ambalo limewasukuma katika kubuni
miradi ambayo itawawezesha kumudu maisha na changamoto zake.
Mmoja wao, Simon Kinabo, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichoko Morogoro ameamua kujiajiri baada ya kubuni mradi wa ufugaji wa samaki.
Mradi
huo unaoitwa Rombo Unique Aquaculture, upo kilomita 60 kutoka mjini Moshi
na kilomita nne kutoka makao makuu ya Wilaya ya Rombo, eneo la Mkuu.
Anasema akiwa mwanafunzi katika chuo hicho, akisomea Shahada ya Sayansi ya Viumbe wa Majini (BSc Aquaculture) alihamasika na somo la uzalishaji wa samaki na ndipo akaamua kuanzisha mradi huo kwa mtaji wake.

“Katika
fedha zile za mkopo, kila nikipewa na Serikali, nilichukua kiasi kidogo
na kuanzisha nyumbani mradi wa kufuga samaki.
Niliamini ni mradi mzuri ambao unaweza kubadili maisha yangu,” anasema.
Anaongeza kuwa alianzisha mradi huo kwa kuchimba bwawa dogo na kuanza kuzalisha samaki, kwa lengo la kuja kuwauza baadaye.

Mkopo
wa CRDB
Anasema akiwa mwaka wa pili SUA alipata taarifa ya kuwapo mradi wa SUGECO unaoendeshwa na chuo hicho na CRDB ambao unalenga kuwawezesha wanafunzi wa elimu ya juu kuingia katika ujasiriamali.

“Baada
ya kupata taarifa hizo nilijitokeza kuandika andiko la kuomba fedha na baada ya
usaili, andiko langu lilipitishwa na chuo na CRDB,” anasema.
Anaongeza kuwa baada ya kupitishwa andiko lake, alipokea mkopo wa Sh20 milioni kwa ajili ya kuanzisha mradi.

Baada
ya kupokea fedha, aliamua kupanua bwawa hilo na pia kuliongezea mifumo ya
kuingiza maji kutoka Mto Ngwasi na kutoamaji ili liwe la kisasa.
“Nilinunua mabomba 100 ya futi 2,000 na sasa bwawa langu lina urefu chini, mita tatu hadi sita na upana mita 30,” anaeleza.

Anasema
kuwa baada ya upanuzi wa bwawa alinunua samaki wadogo 3,000 kutoka Gereza la
Karanga mjini Moshi ambao walikuwa ni wa jamii ya perege na kambare.
Anaongeza kuwa kila kifaranga cha samaki alikinunua kwa Sh300 na kwamba hiyo ilikuwa Mei 5, mwaka jana, alipoanza kuwapandikiza bwawani mwake.

Mafanikio
ya mradi
Hadi sasa, Kinabo anasema bwawa lake linao zaidi ya samaki 40,000, kati ya hao wakubwa ni 10,000 na wadogo 30,000.
Anasema , Juni mwaka huu anatarajia kuanza kuvua samaki na matarajio yake ni kuvua tani nne za samaki.
“Nina imani tani hizo nne, nikivua naweza kupata zaidi ya Sh60 milioni na tayari nimepata masoko,” anasema msomi huyo.

tayari, amefanya mazungumzo na wakuu wa shule kadhaa za sekondari
wilayani Rombo, Hospitali ya wilaya hiyo na maeneo kadhaa ambao wamekubali
kununua samaki wake.
Kwa
kutambua kuwa hawezi kufanya kazi hizo peke yake, mjasiriamali huyo msomi
amemwajiri mtunza mazingira, James Edmund, pia hivi karibuni atakuwa na
walinzi wawili na muuzaji wa samaki.
kwa hisani yamwanachi