Hali ya ulinzi na usalama katika mazingira ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imezidi kuwa mbaya kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya wizi na ukabaji.Mara hii imefikia pabaya zaidi kwani wezi wamekuwa wakitumia silaha kama mapanga na visu kufanyia uhalifu huo na tumekuwa tukishuhudia wenzetu wakijeruhiwa vibaya na kuporwa mali zao kama laptop,fedha au simu.Cha kusikitisha uhalifu huo umefikia kwenye hatua ya ubakaji kwani tumesikia dada yetu mmoja amepatwa na mkasa huo hivi karibuni.Tunawapa pole wote waliopatwa na maswahibu hayo.Tujiulize hawa wanausalama wetu (auxiliary police) wako wapi wakati haya yanatokea?Vipi management ya chuo inafahamu haya?wamejipanga vipi kutuhakikishia usalama wetu?
|
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa safari ya kifo cha kijana huyo ambae hakujulikana jina. |
Kwali hali hii,hatua za makusudi inabidi zichukuliwe haraka,kwani cha kutisha wamekuwa wanaingia kwenye hostel (hall of residence) bila woga.Ni hivi karibuni tu Hall 5 na Hall 2 wamekamata na kuwapa kipigo wezi hao kisha kuchukuliwa na Auxiliary Police,lakini hatujui hatma yao.Labda hatua za kisheria zinaendelea?!!Kama ndivyo,basi inabidi zifanyike haraka na umma kupewa taarifa kwani maafa yaliomkuta mwizi wa juzi yametokea kutokana na kuona sheria hazitekelezwi hivyo wanafunzi wakaamua kuchukua sheria mkononi.Lakini tujiulize kumuua mwizi ni suluhisho la tatizo hili?
Japokuwa inauma sana kuona wenzetu wanapata ulemavu, kupoteza mali za thamani na muda wa masomo kutokana na uhalifu waliofanyiwa na wezi hawa,lakini kitendo cha kumpiga na kumtesa mtu hadi kufa ni kitendo cha kinyama kisicho na utu hasa kwa wasomi wa chuo kikuu.Hata maandiko yameandika “alipizae ubaya kwa ubaya huyo ni shetani”, “isitoshe akupigae shavu la kulia mgeuzie la kushoto’.Hata katika sheria za uislamu (Islamic Sharia) adhabu ya mwizi imesemwa ni kukatwa mkono na sio kifo!kwanini tusingeamua hata kufuata sheria hii labda ingeweza kuwa funzo? Thamani ya uhai wa mtu hailinganishwi na kitu chochote.
|
Tutafakari kwanini yule binti wa Kizungu alipiga kelele “stop it,stop it, it’s against human rights” nahisi hakuwahi kuona katika maisha yake unyama kama ule, pia hakuwahi kudhani mwanadamu wenye akili timamu anaweza kufanya vile.Japo tulimdhihaki kwa kumwambia “eti Human rights unazijua leo,wakati mnawatesa babu zetu enzi za slave trade hamkuziona??”tukamtimua eneo la tukio!!hapo ndipo tulipodhihirisha udogo wetu wa kufikiri na kwamba elimu tunayoipata haijatukomboa.Inabidi tukubali kwamba its completely against humanity. Yatupasa kutubu kwa Mungu na dhambi ile isitutafune.
|
Binti wa kizungu aliyejaribu kutetea uhai wa kijana yule. |
Tujiulize tumefanya vile kwanini?ni kulipiza kisasi au ni kwa kujipoza kwa maswahibu yalowakuta wenzetu au ni kutoa funzo kwa wezi wengine??Hofu yangu ni kwamba wezi hawa wakiamua kuungana na kulipiza kisasi kwa mauaji yaliompata mwenzao na uhakika tutakuwa katika hali ya hatari zaidi!!Wao wana uwezo zaidi,wakiamua kutuwinda kwa mishale au kuja kutuchomea moto tukiwa hosteli??! MUNGU AEPUSHE MBALI BALAA HIZI!! Kweli usalama wetu ni mdogo na hatari ipo kwetu zaidi. Vita hiyo hatutoiweza.Tunahitaji sheria madhubuti ambazo zitatoa adhabu kali na kuwa fundisho kwa wahalifu,kwani imeonekana kuwa ongezeko la kuchukua sheria mkononi ni kutokana wananchi kuchukizwa na hali ya wahalifu kuachiliwa huru bila kupewa adhabu yoyote.Na imani kwa sala ya mwisho aliyoombewa na dada yetu kabla ya kukata roho, marehemu mwizi atapumzika kwa amani.
|
Akiwa tayari amekata roho!! |