
Mwandishi wa habari hizi ambaye hufanya ziara za kusaka matukio ya kijamii kwenye vijiji mbali mbali vya mji wa Morogoro, alipokutana na mzee Juma kwenye msitu huo alimsimamisha na kuhojiana naye na ndipo mzee Juma alisema mtoto wake huyo, Athuman Mohamed (5) alikuwa akisumbulia na homa, hivyo alimua kumpeleka kwenye zahanati aliyodai iko umbali wa takribani kilometa 10.
“Jana usiku hatukulala. Amejiwa na homa kali hivyo kutokana na umbali wa safari niliamua kumsafirisha kwa kumuweka kwenye tenga ninalotumia kuvunia nyanya shambani... umri wake mdogo...alikuwa akitetemeka sana kwa homa kali, kama angeketi kwenye kiti cha baiskeli usalama ungekuwa mdogo... mama yake alishauri nimfunge kwenye tenga, " alisema mzee Juma.
Picha na stori kwa hisani ya wavuti
No comments:
Post a Comment