Lema ashinda rufaa ya kesi yake



Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema leo ameshinda rufaa ya kesi yake. Mahakama  imejiridhisha kuwa madai ya udhalilishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM).
Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel.Kufuatia  sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema.

No comments: