Awamu nyingine ya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO UDSM) imeanza kwa kasi kwa wagombea kunadi sera katika kampeni zilizoanza tokea jumapili tarehe 12 Juni,baada ya kutangazwa majina ya wagombea waliopitishwa tume ya uchaguzi ya chuo kikuu.
Wagombea waliopitishwa kwa upande wa urais ni Shukuru Mlwafu,Saimon Kilawa na Richard Damas,na kwa nafasi ya makamu wa rais ni Angelista Noshan na Gift Msowoya
Picha za wagombea katika moja ya kuta maeneo ya SJMC. |
Mchakato huo ni mzito hivyo ni ngumu sana kutabiri mshindi ni nani kwani wagombea wote wameonekana kuugwa mkono kwa kiasi kikubwa. “Mchuano ni mkali sana hivyo ni ngumu kusema nani atakuwa Rais wetu,kazi hiyo tumeuwashia umma wa UDSM” anasema Mwanaharati mkongwe Rich.
Kama ilivyo kawaida ya siasa hali ya kuchafuana imekuwa ikijitokeza kwani baadhi ya wagombea wamekuwa wakishutumiwa kuwa makada wa CCM ingawa haijathibitishwa.Kwa upande wengine kivutio kikubwa kimejitokeza kwa upande wa nafasi ya makamu wa rais kwani wagombea wote wanamvuto wa sura hivyo watu wamekuwa wakihoji kama mvuto ni moja ya kigezo kilichotumika kuwapitisha katika mchujo uliofanyika.
Hawa wagombea wa nafasi ya makamu wa rais na sio washiriki wa urembo kama wanavyodhaniwa |
Mfuasi wa Bw Mlwafu Shukuru akiwa amebeba bango la kumnadi. |