Zikiwa zimebakia siku chache kwa
matokeo ya kidato cha sita 2012 kutoka, “homa” juu ya
hatima ya vijana waliofanya mtihani huo imezidi kuongezeka. Joto hili limezidi
kuongezea sio tu kwa kuhofia ufaulu wa mtihani yao bali kilichoongeza sintofahamu
ya hatma yao kwenda vyuoni, wengi
wahofia kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu kwani hali ya kupata ufadhili
kutoka bodi ya mikopo (HESLB) umeanza kuonekana kuwa mgumu (tete).
Kukata tamaa huku kumechangiwa zaidi na
taarifa zilizotolewa na TCU kupitia kitabu cha mwongozo wa udahili
2012/2013-Admission guide book 2012/2013. Katika kitabu hicho ambacho licha ya
kutoa vigezo vinavyohitajika ili mwanafunzi achaguliwe kwenda kusoma katika
chuo husika pia wametoa mchanganuo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo
2012/2013. Katika mchanganuo huo unaonyesha vipengele viwili ambavyo ni Possible
Loan amount na Loan Priority. Katika kipengele cha loan priority kinaonyesha kozi (taaluma) ambazo zimepewa kipaumbele
cha kupewa mkopo, hivyo kupelekea kuwepo kwa makundi mawili ambayo ni Priority na Non Priority. Kwa ufupi non priority ni wale ambao hawana uwezekano
wa kupata mkopo. Hivyo possible loan
amount kinawahusu wale ambao ni priority
(watakopata mkopo)
Cha kusikitisha zaidi, ni kwamba asilimia
96 ya kozi zote zinazotolewa na vyuo mbalimbali ni non priority isipokuwa kwa wataochagua Education, Engineering na Medicine,Kilimo na kozi nyingine baadhi
za sayansi. Hiki ni kizungumkuti kwa
wale waliokuwa na matumaini ya kusoma Biashara, Uchumi, Political Science,
Sheria, Uandishi wa Habari, na kozi nyingine zilizobaki kwani upatikanaji wa
mikopo kwao ni ndoto. Sijui ndugu zangu watoto
wa wakulima waliosoma EGM, HGE, HKL, HGL, HGK KLF nk watakimbilia wapi? Kimbilio
liliobaki ni education pekee, tena watakaomudu
kusoma hii ni wale waliotoka kwenye
familia zenye auheni kidogo (middle class) kwani bodi wanatoa ufadhili wa 50%
kwa watakaosoma education; lakini kwa mtoto wa mkulima choka
mbaya kupata elimu ya chuo asahau.
Wazee wa IFM mpo??chuoni kwenu hakuna kozi hata moja inayokula mkopo?? |
Uwezo wa kumudu gharama za ada, (tuition fee), chakula
na malazi (meals & accommodation), na fedha nyingine za kujikimu
zitapatikana wapi? Gharama hizi mzigo usiobebeka na wazazi wengi hawawezi
kumudu gharama hizi. Hiki ni kilio, tena kisicho na mfiwa maalumu..wafiwa ni
watoto wa masikini ambao ni tuko wengi hapa Tanzania. Kwa hali hii watakaosoma
vyuo ni watoto wa matajiri tu! watoto wa wakulima twende wapi? kwenye mabenki tukachukue mikopo ya
kujisomesha? Inasikitisha kuangalia kitabu hicho cha TCU.
Hii ni chinja chinja mpaka wazee wa Mzumbe panga hili limewapitia |
Nashindwa kuelewa nini maana ya
mkopo?hivi fedha hizi si hurudishwa pindi mwombaji anapomaliza masomo? Au ndo
serikali haina fedha kama tunavyosikia? Huku ni kutowatendea haki watoto wa
masikini walio na kiu ya kupata elimu ya juu. Tena ni uonevo mkubwa..njooni
vyuoni mtazame maisha ya wanafunzi wa mwaka jana waliokosa mkopo..maarufu kama NO LOAN…nadhani kupitia hili umuhimu wa
kuwapatia wanafunzi mikopo unaweza kuonekana.
Sio kwenu tu IFM ndo hakuna mkopo?vyuo kibao kama CBE,Ustawi, Tumaini,KIU,bodi hawatoi mkopo pia |
Matokeo hayo ya kidato cha sita yanatarajiwa kutoka mwisho mwa mwezi huu kama ilivyo ada.
Wazee wa SUA |
HILL mpo?? |