Kwa muda mrefu sasa hapa Tanzania tunakabiliwa na tatizo la mgao wa umeme bila kujua chanzo chake ni nini wala mwisho wake ni lini. Kama mmoja wa waathirika wa tatizo hili,wakati nikitafakari kuhusu tatizo hili, kwa kuona uzito wake, nikasema sio bure labda nchi yetu na shirika la umeme TANESCO wamelogwa!!nikaona HAPANA kwa waganga tulionao hapa nchini ufumbuzi ungekuwa umeshapatikana mapema. Ghafla nikapata jibu kwamba shirika la TANESCO limelaaniwa! ndiyo limelaaniwa. Sasa laana hii imetoka wapi? Nikakumbuka ule mgogoro wa TANESCO na Askofu Zachary Kakobe kuhusu kupitisha kanisani kwake nguzo za umeme zenye kilovoti 132 uliojitokeza mwanzo mwa mwaka 2010, Askofu Kakobe pamoja na wamumini wake walikesha na kufunga kwa maombi ili nguzo za Tanesco zisipite kanisani kwako lakini Tanesco walitumia nguvu ya serikali wakapitisha nguzo, Kakobe hakuridhia uamuzi ule na aliahidi kuuendelea na maombi ili kuwaaibisha TANESCO na aliongeza kuwa kwamwe hawataweza (TANESCO) kushindana na Mungu, (baba wa sayansi zote). Mungu hawezi kupuuzia sala na maombi ya wale Vikongwe waumini na Kakobe waliokesha usiku na mchana kulinda kanisa lao ili TANESCO wasipitishe nguzo. HAKIKA SASA MAOMBI NA SALA ZA MTUMISHI WA MUNGU KAKOBE zimesikika MBINGUNI, TANESCO imeshindwa kabisa kutatua tatizo la umeme nchini.
Askofu Kakobe wakati wa mgogoro wake na TANESCO mwaka jana |
Kudhihirisha hilo kuwa laana hii yatoka kwa MUNGU kama alivyosemwa katika maandiko “nitakulaani wewe na vizazi vyako vyote” ni kweli sasa imekuwa sio kwa TANESCO tu, bali laana hii imeenea kwa wizara yote ya nishati na madini. Angalia mgogoro wa ukosefu wa mafuta nchini uliojitokeza hivi karibuni, kutoelewana kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na EWURA, kusimamishwa kazi kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw Davis Jairo na hata kupingwa kwa bajeti ya wizara kutokana na tatizo la umeme. Yote haya yanadhihirisha kwa kizazi chote cha wizara ya nishati na madini vimekumbwa na laana hii.
Tatizo la mafuta lilivyojitokeza hivi karibuni. |
Ili kuondokana na haya yote, TANESCO wamrudie Kakobe na awaongoze kwa sala ya toba. Kama walivyofanya kipindi kile cha mgogoro, Waziri Ngeleja na serikali kwa ujumla itawalazimu tena wamrudie mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe ilikupata baraka zake, la sivyo tatizo la umeme litaendelea licha ya serikali kuonyesha nia ya dhati ya kutatua tatizo hili.
Askofu Kakobe na Waziri Ngeleja wakati wa mgogoro kuhusu wa uwekaji nguzo. |