You are beautiful in your color!!

Nikiwa katika mihangaiko ya kazi nikaenda kwenye ofisi moja maeneo ya Ubungo. Nilipokelewa na mama mmoja (mlinzi) wakati ananipa utaratibu nilikuwa na mshangaa kwa masikitiko kwa jinsi alivyoharibika uso wake (kaungua na kuweka ukungu mweusi). Kwa nyakati hizi imekuwa kawaida kukutana na watu wa aina hii wengine utawakuta ni weupe kupitiliza, wengine wekundu, wengine wamebabuka yaani balaa tupu! sio tu akina dada bali hata akina kaka nao wamejiingiza katika matumizi ya Creams.
Moja ya wanawake walioharibika kutokana na matumizi ya vipodozi pic by modernghana

      Creams ninazozitahaja hapa ni lightening (bleaching) creams ambazo zime-contain mercury and hydroquinone, alpha hydroxyl acids, Arsenic,na nyinginezo nyingi.Kutokana na utafiti wa Dr S Allen Counter 2003 ilionekana kuwa sumu ya mercury (zebaki) imekutwa kwenye miili ya watu wengi wao wakiwa wanawake. Nchi zilizooneka kuwa vinara katika hili ni Mexico,Saudi Arabia, Senegal,Tanzania na nchi nyingine za Afrika magharibi. Sababu kubwa unayowafanya watu kuji-cream (kujichubua) ni kwa ajili kwa kutaka kuonekana warembo. Lakini hii ni kasumba mbaya kwani kuwa mrembo au kuonekana unapendeza ni lazima uwe mweupe? HAPANA tena tafiti zinaonyesha kuwa most beautiful and attractive women in the world are actually black women! Angalia akina Naomi Campbell, Halle Berry, Tyra Banks,Miriam Odemba, Nancy Sumari na wengine wengi. Kibaya zaidi tunaambiwa “Beauty is more than skin deep” . Athari kubwa zimekuwa zikionekana sana huku kwetu Afrika kwa sababu vipodozi hivi vingi haviko favorable na mazingira yetu kwani watngenezaji wanashauri watumiaji wasiwe wanakaa jua au watumie sunblock masharti haya wengi wa akina dada zetu yamewashinda!! Hivyo kujikuta wanababuka ngozi zao,  athari nyingine ambazo zinazowatokea ni kuzeeka kwa ngozi kutokana na mikunjo hivyo kumfanya kijana anaonekane mzee, kupata cancer hali kadhalika kifo chaweza kutokea kwa wale wanaofanya  plastic surgery.
Nancy Sumari one of the black beautiful girl
  Licha ya vipodozi hivi kupigwa marufuku katika nchi mbalimbali lakin bado vimekuwa vikiuzwa  kinyemela.Imeshauriwa kuwa watumiaji waepuke vipodozi vyenye chemical hizo au watumie vipodozi vya asili (HERBAL) ambavyo vinaweza kulinda urembo wao.
Jikubali ulivyo because you are beautiful in your natural color.

VOTE FOR Mt KILIMANJARO


   Ukiwa kama mdau wa unahimizwa kuuwezesha mlima Kilimanjaro kushinda na kuwa moja ya maajabu ya dunia. Hii ni kupitia shindano la new 7 world wonders linaloendeshwa hivi sasa. Mlima Kilimanjaro una mita 5895 kutoka usawa wa bahari  (5895 from the sea level)  una vigezo vyote vya kuingia katika  new world wonders, kwanza   kabisa ni mlima mrefu kuliko yote barani Africa, pia una vilele viwili ambavyo ni Kibo na Mawenzi zaidi ni kwamba, inastaajabisha kwa mlima kama huu (Volcanic mountain)  kuweko katika ukanda wenye hali ya hewa ya Kitropiki.
 Kuupigia kura ni rahisi tembelea www.new7wonders.com au bofya  hapahttp://www.new7wonders.com/vote-2?lang=en
      Lets unite & enable mount Kilimanjaro to be the new world wonder.

SIRI YA MGAO WA UMEME NCHINI HII HAPA


   Kwa  muda mrefu sasa hapa Tanzania tunakabiliwa  na tatizo la mgao wa umeme bila kujua chanzo chake ni nini wala mwisho wake ni lini. Kama mmoja wa waathirika wa tatizo hili,wakati nikitafakari kuhusu tatizo hili, kwa kuona uzito wake, nikasema sio  bure  labda nchi yetu na shirika la umeme TANESCO  wamelogwa!!nikaona HAPANA kwa waganga tulionao hapa nchini ufumbuzi  ungekuwa umeshapatikana mapema. Ghafla nikapata jibu kwamba shirika la TANESCO limelaaniwa! ndiyo limelaaniwa. Sasa laana hii imetoka wapi? Nikakumbuka  ule mgogoro wa TANESCO na Askofu Zachary  Kakobe kuhusu kupitisha kanisani kwake nguzo za umeme zenye kilovoti 132 uliojitokeza mwanzo mwa mwaka 2010, Askofu Kakobe pamoja na wamumini wake walikesha na kufunga  kwa maombi ili nguzo za Tanesco zisipite kanisani kwako  lakini Tanesco walitumia nguvu ya serikali wakapitisha nguzo, Kakobe hakuridhia uamuzi ule na aliahidi kuuendelea na maombi  ili  kuwaaibisha TANESCO na aliongeza kuwa kwamwe hawataweza (TANESCO) kushindana na Mungu, (baba wa sayansi zote). Mungu hawezi kupuuzia sala na maombi ya wale Vikongwe waumini na Kakobe waliokesha usiku na mchana kulinda kanisa lao ili TANESCO wasipitishe nguzo. HAKIKA SASA MAOMBI NA SALA ZA MTUMISHI WA MUNGU KAKOBE zimesikika MBINGUNI, TANESCO imeshindwa kabisa kutatua tatizo la umeme nchini.

Askofu Kakobe wakati wa mgogoro wake na TANESCO mwaka jana
      Kudhihirisha hilo kuwa laana hii yatoka kwa MUNGU kama alivyosemwa katika maandiko “nitakulaani wewe na vizazi vyako vyote” ni kweli sasa imekuwa sio kwa TANESCO tu, bali laana hii imeenea kwa wizara yote ya nishati na madini. Angalia mgogoro wa ukosefu wa mafuta nchini uliojitokeza hivi karibuni, kutoelewana kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na EWURA, kusimamishwa kazi kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini  Bw Davis Jairo na hata kupingwa kwa bajeti ya wizara kutokana na tatizo la umeme. Yote haya yanadhihirisha kwa kizazi chote cha wizara ya nishati na madini vimekumbwa na laana hii. 

Tatizo la mafuta lilivyojitokeza hivi karibuni.
     Ili kuondokana na haya yote, TANESCO wamrudie Kakobe na  awaongoze kwa sala ya toba. Kama walivyofanya kipindi kile cha mgogoro, Waziri Ngeleja na serikali kwa ujumla itawalazimu tena wamrudie mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe ilikupata baraka zake, la sivyo tatizo la umeme litaendelea licha ya serikali kuonyesha nia ya dhati ya kutatua tatizo hili.
Askofu Kakobe na Waziri Ngeleja wakati wa  mgogoro kuhusu  wa uwekaji nguzo.

TCU YATOA TAMKO KWA FORM SIX LEAVERS.


  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewataka wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kupitia tume hiyo kuwa na uvumilivu kwani majibu yatatoka hivi karibuni.

   Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Uhusiano wa TCU, Edward Mkaku, alipozunguumza na gazeti la NPASHE ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya wanafunzi walioomba nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwamba tume imechelewa kutangaza majina.

   Mkaku alisema kwa kawaida matokeo ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini hutolewa mwishoni mwa Julai. Hata hivyo, alisema mwaka huu majina yamechelewa kutangazwa kwa kuwa Seneti za vyuo zimechelewa kufanya vikao kwa ajili ya kupitia na kuhakiki majina na sifa za walioomba.

   Alisema kazi ya TCU ni kuratibu na inapomaliza humuita Afisa Msajili wa kila chuo kwenda kuangalia kama wanafunzi waliochanguliwa wana vigezo vya kujiunga na chuo husika kwa kuwa kila chuo kina kuwa na vigezo vyake. Baada ya kila Afisa Msajili kuhakiki vigezo vya waliochanguliwa, huenda kukaa na Baraza la Seneti la kila chuo kuhakiki tena vigezo hivyo na baada ya hapo majibu yanarudishwa TCU.

  Akasema TCU ilikutana jana na wakati wowote itatoa majibu ya waliochanguliwa kujiunga na vyuo vikuu.

Alisema TCU ina mawasiliano ya vyuo hivyo ambavyo ni taasisi huru.

from,wavuti.com 

HII NDIYO AFRIKA YETU.

    Naamini bara la Afrika ni moja ya sehemu iliyobarikiwa sio tu kwa rasilimali zilizopo bali pia kuwa na watu wenye nguvu kuliko sehemu nyingine duniani. Lakini cha ajabu ndio sehemu inayoongoza  kwa matatizo kama vita (vurugu),ufukara,ufisadi,njaa na ukame kuliko sehemu  yoyote.Sijui tatizo letu ni nini??. Wapo wanaosema eti WAAFRIKA TUMELAANIWA!! Mimi siamini kwamba tumelaaniwa kwani Mungu hawezi kuwa katili na muonevu kwa Waafrika kiasi hicho,tatizo lipo sehemu limejificha,kuzungumzia LAANA ni uvivu wa kufikiri  na uwoga wa kuumiza kichwa katika ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili.


    Kwa upande mwingine inaniingia akilini kwamba yaweza kuwa laana,tena iliyotoka kwa shetani, hii inatokana na matendo yatunayofanya waafrika. Mfano mzuri ni hali inayoendelea huko pembezoni mwa afrika katika nchi ya Somalia,kwa muda wa miezi mine sasa imekumbwa na ukame na njaa illiyosabisha njaa kali kwa wananchi na mifugo yao. Hali hii imesababisha vifo vya mamia ya watu hasa watoto na wengine maelfu kukimbilia nchi za Kenya na Ethiopia kama wakimbizi.

Baadhi ya wakazi wa Somalia waliokimbilia Kenya
   
 Kutokana na hali hii mashirika ya kibinadamu kama Save the children wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwa wakimbizi kwa wananchi wa Somalia na wamekuwa wakitoa taarifa kuwa hali inazidi kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba wafanyakazi wa shirika hili wamekuwa wakivamiwa na waasi hivyo kukwamisha zoezi la utoaji wa misaada. Hata baada ya umoja wa maataifa kupitia shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mradi wa chakula duniani (World Food Programe) kuamua kwenda kutoa  misaada ya chakula,waasi hawa wa Alshabab wameanzisha mapigano makali dhidi ya mashirika haya,huko mjini Mogadishu.

Mama wakisomali akiwa na mwanae
   Hakika huu ni ukatili wa hali ya juu,licha ya kuona wenzao(ndugu zao) wanasulubika kwa tatizo la njaa bado wameamua kuwazuia kupata chakula hicho. Nahisi lengo lao ni kuwamaliza kabisa.Kwanini waafrika tumekosa utu na huruma kwa wenzetu? Kwa hali hii zoezi la kuwanusuru ndugu zetu wasomali na baa hili la njaa limeingia dosari,hivyo tuzidi kuomba miujiza ili Alshabab wasitishe mapigano na watoto,vijana na wazee wa Somalia wanusurike na njaa inayowakabili.
  

HAVE YOU THOUGHT THIS??

Hapa kwetu Tanzania tumezoea kusikia  mtu akiwa chuo basi anasoma sheria, udaktari, engineering, uhasibu, Human Resources( HR) au Ualimu lakini hii tofauti kwa wenzetu kwani  hutumia  gharama kubwa kusomea fani nyngine mfano mapishi..

I thought making ice-cream was pretty easy, but it seems that if you really want to get it right you have to take courses at the Gelato University, in Bologna, Italy.

Lango la kuingilia chuoni hapo.
  Ice-cream making was one of the last thing I would have imagined required attending a university, but in reality thousands of students from all over the world study the art of making quality ice-cream at the Carpigiani Gelato University, in Bologna, every year. Gelato lovers, and entrepreneurs who want to learn the secrets of making great ice-cream and take it back to their homelands pay around €800 ($1,138) for a week of courses and accommodation at a nearby hotel. They attend technical lectures on traditional gelato-making techniques by veteran ice-cream makers, and take part in practical courses where they learn to use the world famous Carpigiani gelato machines.

Hapa ni baada ya Presentation yao.

Believe it or not, the Carpigiani Gelato University has been around for a long time, and as more people around the globe fall in love with the Italian gelato, it gets more students with each passing year. In 2011, the number of students has gone from 9,000 to 12,000 and for the first time in history, the number of foreign tourists has surpassed that of Italians.
  
Washikaji wakiwa katika lecture  fromhttp://odditycentral.com

HII INA KUHUSU MTUMIAJI WA INTERNET!!

  Katika dunia ya sasa suala mifumo ya upokeaji wa taarifa  na mawasiliano (information and communication technology-ICT) kwa sasa limekua sana, sio tu kwa nchi zilizoendelea hata kwa nchi zinazoendelea mfano mzuri ni hapa nyumbani Tanzania,tumeona kwa kiasi chake maendeleo ya mifumo ya digitali na satelaiti( digital & satelite),na intanet vikiongezeka kwa kasi.Chakusikitisha ni kwamba badala ya maendeleo haya kutusaidia kusonga mbele,sasa yamegeuka kikwazo cha sisi kufikia maendeleo yanayohitajika kwa mfano uwepo wa intaneti sio  tu kwa kutuvunjia maadili bali hata kwa kutupotezea muda mwingi wa kufanya shughuli nyingi za kimaendeleo.Kwani hivi sasa watu hutumia muda mwingi ku-chat kwenye facebook au twitter.Kibaya zaidi kinachozungumzwa humo ndani ni upuuzi usiojenga.

Jamaa kakomaa na surakitabu       (pic wavuti.com)
    Kwa wenzetu vitu vinawasaidia sana sio tu katika mawasiliano bali hata kutangaza biashara zao,katika elimu (online education) na zaidi hata kutoa nafasi za ajira.Tofauti kabisa na hapa kwetu,bado tuna ile kasumba ya kizamani ya kuhisi kuwa facebook ipo kwa ajili ku-upload picha tu.Unaweza kukuta mtu amekesha internet lakini anachokifanya hakina manufaa.Imefika wakati tubadilishe mitazamo yetu,tutumie vyombo hivi kwa namna itakayotuletea manufaa.

THIS IS TOO MUCH!!

    Tafiti nyingi zilizokwishafanyika zinaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa nyani na wanyama wengine jamii ya sokwe wanafanana na binadamu sio tu kwa sura(muonekano),mfumo wa uzazi halikadhalika matendo yao kwani mambo yote anayofanya binadamu nao nyani wanauwezo wa kufanya vizuri.  
Hapa ameshika bunduki aina ya AK 47! (www.wavuti.com)
Hapa sijui anafikiria familia yake??!!

   Wataalam wanasema tofauti iliyopo kwamba binadamu ana uwezo mkubwa(IQ) wa kutambua mambo kuliko nyani.Pia tendo aliloweza nyani ni kuzungumza(produce sound speech).


VITA HII UDSM MPAKA LINI??

  Hali  ya ulinzi na usalama katika mazingira ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imezidi kuwa mbaya kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya wizi na ukabaji.Mara hii imefikia pabaya zaidi kwani wezi wamekuwa wakitumia silaha kama mapanga na visu kufanyia uhalifu huo na tumekuwa tukishuhudia wenzetu wakijeruhiwa vibaya na kuporwa mali zao kama laptop,fedha au simu.Cha kusikitisha uhalifu huo umefikia kwenye hatua ya ubakaji kwani tumesikia dada yetu mmoja amepatwa na mkasa huo hivi karibuni.Tunawapa pole wote waliopatwa na maswahibu hayo.Tujiulize hawa wanausalama wetu (auxiliary police) wako wapi wakati haya yanatokea?Vipi management  ya chuo inafahamu haya?wamejipanga vipi kutuhakikishia usalama wetu?

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa safari ya kifo cha kijana huyo ambae hakujulikana  jina.
 Kwali hali hii,hatua za makusudi inabidi zichukuliwe haraka,kwani cha kutisha wamekuwa wanaingia kwenye hostel (hall of residence) bila woga.Ni hivi karibuni tu Hall 5 na Hall 2 wamekamata na kuwapa kipigo wezi hao kisha kuchukuliwa na Auxiliary Police,lakini hatujui hatma yao.Labda hatua za kisheria zinaendelea?!!Kama ndivyo,basi inabidi zifanyike haraka na umma kupewa taarifa kwani maafa yaliomkuta mwizi wa juzi yametokea kutokana na kuona sheria hazitekelezwi hivyo wanafunzi wakaamua kuchukua sheria mkononi.Lakini tujiulize kumuua mwizi ni suluhisho la tatizo hili?

    Japokuwa inauma sana kuona wenzetu wanapata ulemavu, kupoteza mali za thamani  na  muda wa masomo kutokana na uhalifu waliofanyiwa na wezi hawa,lakini kitendo cha kumpiga na kumtesa mtu hadi kufa ni kitendo cha kinyama kisicho na utu hasa kwa wasomi wa chuo kikuu.Hata maandiko yameandika “alipizae ubaya kwa ubaya huyo ni shetani”, “isitoshe akupigae shavu la kulia mgeuzie la kushoto’.Hata katika sheria za uislamu (Islamic Sharia) adhabu ya mwizi imesemwa ni kukatwa mkono na sio kifo!kwanini tusingeamua hata kufuata sheria hii labda ingeweza kuwa funzo? Thamani ya uhai wa mtu hailinganishwi na kitu chochote.

    Tutafakari kwanini yule binti wa Kizungu alipiga kelele “stop it,stop it, it’s against human rights” nahisi hakuwahi kuona katika maisha yake unyama kama ule, pia hakuwahi kudhani mwanadamu wenye akili timamu anaweza kufanya vile.Japo tulimdhihaki kwa kumwambia “eti Human rights unazijua leo,wakati mnawatesa babu zetu enzi za slave trade hamkuziona??”tukamtimua eneo la tukio!!hapo ndipo tulipodhihirisha udogo wetu wa kufikiri na kwamba elimu tunayoipata haijatukomboa.Inabidi tukubali kwamba its completely against humanity. Yatupasa kutubu kwa Mungu na dhambi ile isitutafune.

Binti wa kizungu aliyejaribu kutetea uhai wa kijana yule.
   Tujiulize tumefanya vile kwanini?ni kulipiza kisasi au  ni kwa kujipoza kwa maswahibu yalowakuta wenzetu au ni kutoa funzo kwa wezi wengine??Hofu yangu ni kwamba wezi hawa wakiamua kuungana na kulipiza kisasi kwa mauaji yaliompata mwenzao na uhakika tutakuwa katika hali ya hatari zaidi!!Wao wana uwezo zaidi,wakiamua kutuwinda kwa mishale au kuja kutuchomea moto tukiwa hosteli??! MUNGU AEPUSHE MBALI BALAA HIZI!! Kweli usalama wetu ni mdogo na hatari ipo kwetu zaidi. Vita hiyo hatutoiweza.Tunahitaji sheria madhubuti ambazo zitatoa adhabu kali na kuwa fundisho kwa wahalifu,kwani imeonekana kuwa ongezeko la kuchukua sheria mkononi ni kutokana wananchi kuchukizwa na hali ya wahalifu kuachiliwa huru bila kupewa adhabu yoyote.Na imani kwa sala ya mwisho aliyoombewa na dada yetu kabla ya kukata roho, marehemu mwizi atapumzika kwa amani.

Akiwa tayari amekata roho!!

Junrey Balawing avunja rekodi ya kuwa mfupi zaidi duniani!

Junrey Balawing raia wa Ufilipino ametangazwa rasmi kuwa mtu mfupi kuliko wote dunia kwa kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikliwa na Khagendra Thapa Magar kutoka Nepal.Junrey ambaye ametimiza miaka 18 hivi karibuni tarehe 11 june ana urefu wa inchi 23.6 sawa na sentimeta 59.93 huku akiwa na uzito wa kilogramu 5,tofauti na Thapa Magar ambaye ana urefu wa 26.4 sentimeta.Kinachofurahisha zaidi ni kwamba amezaliwa tarehe ya uhuru wa nchi yake hivyo inaongeza furaha zaidi kijijini kwao


Pata ukweli zaidi kutoka kwa wazazi:

  At birth, Junrey was the size of a 1-litre coke bottle. His mother only started to suspect something was not right when Junrey was four years old as his friends began to outgrow him. The family sought advice and he was given medication to strengthen his bones, but these made no difference.
  According to his parents, before Junrey was born, his family was poor and down on their luck. But after his birth, they saw a reversal of fortune, with Junrey’s father Reynaldo, 37, getting a job that enabled him to look after his family.  "Junrey is our lucky charm," Reynaldo says.

   Junrey loves watching TV with war films being his favourite viewing also his favourite food is pork but he can eat about two (normal size) fingers' worth at a meal, with a small helping of rice.His name is a combination of June, for his birthday, and his father's name, Reynaldo. It also means "Little King", as in junior and Rey, which is Spanish for king.

  Junrey has to stay at home with his mum Concepcion, while his sisters Jaycel (13), Jeanritch (6) and 11-year-old brother Jay-art go to school. Concepcion (35) says: "He needs my care every minute of every day. Junrey can only walk with some help and he can't stand for too long because he's in too much pain.

  Kutoka na rekodi hii Junrey ameingizwa katika Guinness World Record Book.
                                                                            source;www.guinnessworldrecords.com

MA of Mass Communication launched during SJMC week.

 In celebrating its 50th  anniversary of University of Dar es Salaam through its different colleges has been conducting  events  which aim to expose  its different activities  also to show the success which have achieved for the whole half  century. From Monday 20th of June has been a turn for School of Journalism and Mass communication. The occasion was held at SJMC ground and was honored by the Vice councilor, Prof Rwekaza Mukandala involved the launching of the masters of mass communication programme, which will be offered by University of Dar es Salaam under School of Journalism and Mass Communication.
Prof Mukandala launching MA of Mass Communication at SJMC week

   While presenting the opening speech, Dr Bernadette Killian the Dean of SJMC was able mention problems like accommodation to the students, little number of staff compares to the students’ population also few of resources in Mlimani media.At the same time Prof Mukandala got an opportunity to look over the activities which are done by Mlimani media.


  However the occasion was attended by the former Dean of Tanzania School of Journalism(TSJ) & Institute of Journalism and Mass Communication (IJMC) ,former students,media people and other invited guest.At the end the event was followed by Sports Bonanza which includes table tennis, chicken race, dancing and rope pulling.

A group photo of Prof Mukandala with other invited guest .

                                                   Photos by:Hilal Rihundwa